TANZANIA YASHIRIKI MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII DUNIANI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 21, 2022

TANZANIA YASHIRIKI MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII DUNIANI

 

SERIKALI ya Tanzania inashiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii (FITUR) yanayofanyika katika ukumbi wa IFEMA mjini Madrid, Uhispania.

Tanzania inawakilishwa na  Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa wenye kuwakilisha  Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania pia katika Falme ya Uhispania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (United Nations World Tourism Organisation), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Eneo la Hifadhi la Ngorongoro (NCCA), Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Mamlaka ya Huduma za Misitu (TFS).

Lengo la maonyesho hayo ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika nchi washiriki ili kuinua sekta ya utalii.Maonyesho hayo yalifunguliwa jana tarehe 19 Januari 2022, na Mfalme Felipe VI, ambayo yatahitimishwa tarehe 24 Januari 2022.

Banda la Tanzania limekuwa kivutio kwa kutembelewa na wageni wengi ambao wameonyesha nia ya kutembelea Tanzania bara na visiwani. Maonyesho hayo yanashirikisha nchi zaidi ya 160 na kuhudhuriwa na mawaziri kadhaa wa Utalii kutoka nchi mbalimbali duniani.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad