RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEHUDHURIA TAARAB RASMIN YA KIKUNDI CHA TAIFA KUSHEREHEKEA MIAKA 58 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 13, 2022

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEHUDHURIA TAARAB RASMIN YA KIKUNDI CHA TAIFA KUSHEREHEKEA MIAKA 58 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.


 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita, alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni kuhudhuria hafla ya Taarab rasmin ya kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliofanyika jana usiku,12-1-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amisimama wakati ukipingwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar na Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar, kabla ya kuaza kwa Taarab rasmin  ya kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WASANII wa Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar wakipiga wimbo wa Taifa wa Zanzibar kabla ya kuaza kwa Taarab rasmin ya Maadhimisho ya kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliofanyika jana usiku,12-1-2022 katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Dk.Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwake) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita, wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Bi.Fatma Hamad Rajab, akisoma ratiba ya Taarab Maalum ya kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MSANII Nassor Hussein akiimba wimbo wa Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakati wa hafla ya Taarab Rasmin ya kusherehekea  maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, wakati Kikundi cha Taifa cha Taraab Zanzibar wakitowa burudani, katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakili Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad