HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 13, 2022

Mkandarasi wa Mradi wa Maji wa Kigamboni atakiwa kumaliza kazi kwa wakati

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amemtaka mkandarasi wa mradi wa maji wa Kigamboni mpaka inafika mwezi Aprili mwaka 2022  kuwa ameishamaliza ujenzi wa mradi huo.

Ameyasema hayo alipotembelea mradi wa maji wa Kigamboni unaojumuhisha ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji litakolokuwa na ujazo Lita Milioni 15 pamoja na uchimbaji wa visima katika eneo la Kigamboni.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara hiyo amesema anamtaka mkandarasi wa mradi huo kuendana na muda waliojiwekea na kama akishindwa kuendana makubaliano ya mradi basi watavunja mkataba kwani anawachelewesha wananchi wa Kigamboni kupata maji safi.

"Rais Samia anasisitiza wananchi kupata maji safi na salama lakini inaonekana mkandarasi huyu anataka kukwamisha juhudi zake hivyo hatutaivumilia kasi anayokwenda nayo mkandarasi wa mradi". Alisema Luhemeja.
 
Pia Mhandisi Luhemeja amempongeza Mkandarasi anayetoa maji visimani kwa kukamilisha ununuzi wa pampu tatu za kusukuma maji, huku akimuagiza kuongeza kasi katika mchakato wa manunuzi ya pampu za kutoa maji visimani kupeleka kwenye tenki. 

"Namuagiza Mkandarasi kukamilisha manunuzi hayo mapema ifikapo mwezi wa pili Ili kukamilisha mradi huu, endapo ifikapo mwezi wa nne Mkandarasi hajamaliza mradi tutamwondoa," amesisitiza Mhandisi Luhemeja.
 
Amesema shughuli ya usambazaji wa mabomba kupitia mradi huu wa maji Kigamboni unatarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 17/1/2022  hivyo ametoa maagizo kwa Menejimenti ya DAWASA kuhakikisha wanaendeleza mapambano kukamilisha mradi huu ndani ya Muda.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akikagua Pampu za kusukumia maji zitakazotumika kwenye mradi wa maji wa Kigamboni wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo inatekezwa na DAWASA. Kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi.
Mkurugenzi wa Miradi na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi(kulia) akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu visima vilivyojengwa pamoja na maeneo yatakayojengwa Pampu za kusukumia maji kwenye mradi wa maji wa Kigamboni wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo inatekezwa na DAWASA
Baadhi ya Pampu za kusukumia maji zitakazotumika kwenye mradi wa maji wa Kigamboni
Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Maji Kigamboni, Beda Lyimo akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu wanavyoendelea na ujenzi wa Kituo cha kusukumia maji cha Kimbiji wakati wa ziara yake ya kukagua Miradi ya Maendeleo inatekezwa na DAWASA.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akikagua Tanki litakolokuwa na ujazo wa Lita Milioni 15 kwenye mradi wa maji wa Kigamboni wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo inatekezwa na DAWASA
Muonekano wa tanki la maji litakolokuwa na ujazo wa Lita Milioni 15 linalojengwa kwenye mradi wa Maji wa Kigamboni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutembelea mradi wa maji wa Kigamboni wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo inatekezwa na DAWASA.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad