HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 20, 2021

WAHANDISI WA MITAMBO YA KUONGOZEA NDEGE NCHINI WAKUTANA DAR ES SALAAM

 

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza S. Johari amefungua mkutano wa 24 wa mwaka wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA).

Mkutano huo umefanyika leo Desemba 21 katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock na kuhudhuriwa na wajumbe wa TATSEA, Rais wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA), Mhandisi Francis Asante Chale, pamoja na Wahandisi wasataafu waliokuwa wananchama wa TATSEA.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza S. Johari amesema kuwa, Mamlaka inatambua kwamba Wahandisi wanahitaji kupewa mafunzo yatakayozidi kuwajengea uwezo wa kiutendaji na utekelezaji wa majukumu yao na hivyo Mamlaka hiyo itahakikisha inawapatia wataalam hao mafunzo thabiti yatakayoongeza weledi katika maeneo yao ya kazi.

Johari amesema kutokana na Serikali kununua mitambo ya kisasa ya kuongoza ndege, tunatakiwa kuwa na Wahandisi ambao wamesomea na wamebobea katika kufanya kazi zao pa wahandisi hao wanashughulika na kazi hiyo ya kusimamia mitambo hiyo na kuhakikisha mitambo yote ya kuongozea ndege inafanya kazi masaa 24 na inakuwa kwenye ubora ili kuepusha tatizo la kutopatika kwa mawasiliano ya ndege na kupata ajali.

“Wahandisi hawa wamefanya mradi mkubwa Rada ya kuangazia anga yote ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ili kuhakikisha chombo chochote kinachoruka kinaonekana kwenye mfumo wa Rada.” Alisema Johari.

Pia amewapongeza Wahandisi kwenye mkutano wao kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kuhakikisha mitambo yote inafanya kazi vizuri na ndege zote zikiwa salama kwa kurukasalama bila kugongana huko hewani.

Naye , Rais wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA), Mhandisi Francis Asante Chale amesema wameshiriki mkutano wao wa 24 ili kutathimini kazi zinazofanywa na Wahandisi hao kwa ajili ya kuangalia mabadiliko ya Teknolojia ya vitu mbalimbali vinavyotokea ili wasiwe nyuma.

Amesema maboresho yanayotakiwa kufanyika ni kuendana na Teknolojia ya kisasa kwani kuna mabadiliko makubwa ili kuepusha kutoendana na wahandisi wengine Duniani.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza S. Johari akizungumza kuhusu namna Mamlaka hiyo ilivyojipanga kutoa mafunzi wa Wahandisi wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkutano wa 24 wa mwaka wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA) uliofanyika Desemba 20, 2021 Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akitoa neno kwenye Mkutano wa 24 wa mwaka wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA) pamoja na kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza S. Johari kwa ajili ya kufungua mkutano huo.
Rais wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA), Mhandisi Francis Asante Chale akizungumza kuhusu mikakati ya chama hicho iliyojiwekea pamoja na namna walivyojipanga kwenye Mkutano wa 24 wa mwaka wa TATSEA uliofanyika Desemba 20, 2021 katika ukumbi wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama hai na wastaafu wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA) wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza S. Johari alipokuwa anafungua mkutano mkuu wa Mwaka wa TATSEA uliofanyika Desemba 20, 2021 katika hiteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza S. Johari akitoa zawadi kwa Wanachama wastaafu wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA) wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Mwaka wa TATSEA uliofanyika Desemba 20, 2021 katika hiteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Magreth Kyarenda akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania waliostaafu wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Mwaka wa TATSEA uliofanyika Desemba 20, 2021 katika hiteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza S. Johari akiwa kwenye picha ya pamoja na Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege walohudhuria mkutano Mkutano wa 24 wa mwaka wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA) uliofanyika Desemba 20, 2021 Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza S. Johari akiwa kwenye picha ya pamoja na Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege wastaafu pamoja na wawakilishi mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mkutano Mkutano wa 24 wa mwaka wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA) uliofanyika Desemba 20, 2021 Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad