Na Amiri Kilagalila,Njombe
JUMUIYA
ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Njombe,imefanikiwa
kutekeleza agizo la Chama ngazi ya taifa kwa kujenga nyumba za watumishi
ili kupunguza changamoto za watumishi wa Jumuiya wanapokuwa wamepanga
mitaani.
Akizungumza
baada ya kukagua nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Nzenge halmashauri ya mji
wa Njombe,Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Scolastika Kevela,amesema
jumuiya hiyo wilaya ya Njombe imeonyesha mfano kwa wilaya zote za mkoa
huo na taifa kwa kutekeleza agizo kwa wakati na kuahidi kuendelea
kumuunga mkono mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi taifa kwa vitendo.
“Kwanza
niwapongeze UWT wilaya ya Njombe kwa kazi kubwa mliyoifanya,hili ni
agizo kutoka taifa kwamba tuhakikishe mkoa na wilaya zote tunajenga
nyumba za watumishi wa jumuiya ili kupunguza changamoto za
kupanga”alisema Scolastika Kevela
Ameongeza
kuwa mkoa wa Njombe utaenedelea kuwa bega kwa bega na mwenyekiti wao wa
Chama taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
“Njombe
tuko bega kwa bega na Samia Suluhu na 2025 Njombe tutakuwa na jambo
letu na tutaendelea kumuunga mkono kwa vitendo na huu ndio utendaji
unaoonekana”alisema Kevela
Naye
mwenyekiti wa jumuiya hiyo wilaya ya Njombe Betrece Malekela,amesema
agizo hilo lilitolewa tarehe 23 ya mwezi wa 9 wakiwa Rufiji na kupata
hamasa kubwa ili kumailisha nyumba hiyo kwa wiki tatu pekee na kuwa
miongoni mwa wilaya chache nchini zilizotekeleza agizo hilo.
“Tulipata
hamasa na tukatii maagizo maana ilionekana ni nyumba chache
zilizojengwa kwa nchi nzima,nyumba hii imekamilika ndani ya wiki tatu
wala sio kitu kidogo”alisema Betrece Malekela
Wajumbe
wa baraza la UWT mkoa wa Njombe waliofika na kukagua nyumba
hiyo,wamesema ukamilishaji wa nyumba hiyo umetokana na umoja walio nao
na wilaya ya Njombe imekuwa ni mwanga na kutoa hamasa kwa wilaya
nyingine kutekeleza agizo hilo.
Mwenyekiti
wa UWT mkoa wa Njombe Skolastika Kevela pamoja na wajumbe wa baraza
wakikagua idadi ya vyumba na muonekano wa ndani wa nyumba hiyo iliyopo
mtaa wa Nzenge.
No comments:
Post a Comment