Manispaa ya Tabora yatekeleza Agizo la Rais Samia kutoa Mikopo Mikubwa kwa Vikundi - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 17, 2021

Manispaa ya Tabora yatekeleza Agizo la Rais Samia kutoa Mikopo Mikubwa kwa Vikundi

 

Nteghenjwa Hosseah, Tabora

Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imetekeleza kwa vitendo Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwankutoka mkopo mkubwa utakaoleta tija kwenye vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu. Hayo yamethibitishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake Mkoani Tabora wakati akikagua shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora. Akiwa katika Manispaa hiyo alitembelea Kiwanda cha Kuchakata Asali cha Miombo Neekiping Initiatives kilichopewa Mkopo wa shilingi Milioni 50 zilizowezesha kuanzisha kiwanda ambacho kimetoa soko la uhakika kwa wafugaji takribani 178. Akiwa katika Kiwanda hapo Waziri Ummy amewapongeza vijana hao kwa kuanzisha kiwanda kinachoongeza thamani ya Asali ambayo imewaongezea kipato na pia imesaidia kutoka fursa ya soko la uhakika kwa wafugaji 178. “Sasa nyie muwe vijana wa mfano kwa kuhakikisha kuwa mkopo huu mliopewa ambao hauna riba mnarejesha kwa wakati ili wengine nao waweze kufaidia; Pia aliwataka kutafuta eneo kubwa nje ya Mji ili waweze kujenga Kiwanda kikubwa kwa eneo wilopo sasa ni dogo” Alisema Mhe. Ummy “Niwapongeza Manispaa ya Tabora kwa kutekeleza Agizo hili la Mhe. Rais na kuweza kutoa Mkopo mkubwa kwa kikundi hiki ambao bila shaka Tija ya Mkopo huu tumeshaanza kuiona na sio kama maeneo mengine wanatoa fedha kidogo ambazo hazileti matokeo’ alisisitiza Mhe. Ummy. Wakati huo huo amepongeza Uongozi wa Mkoa kwa hatua nzuri ya waliyofikia katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kukusanya sh. Bil 13.8 sawa na asilimia 51 ya malengo waliyojiwekea ya kukusanya shilingi hil 26.9. Halkadhalika amewapongeza kwa usimamizi makini wa ujenzi wa miundombinu ya madarasa kwani walipokea Fedha Tsh Bil. 1.48 kutoka Mradi wa Maendeleo kwa Ustawi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 60 ya Sekondari na 14 ya vituo shikizi. Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Buriani amesema katika ujenzi wa vyumba vya madarasa Halmashauri za Tabora Manispaa na Nzega Tc wamekamilisha kwa asilimia 100 na halmashauri za Uyui, Urambo,Kaliua na Sikonge wako kwenye asilimia 90 na kwa muda ulioongewa wa tarehe 31 Disemba,2021 watakua wamekamilisha kwa asilimia 100. Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Bw. Peter Maiga Nyanja amesema katika robo ya kwanza wametoa Mikopo yenye thamani ya Mil 273.5 kwenye Vikundi 38 wanawake , 8 vijana na 8 walemavu na katika vikundi hivyo Kikundi cha Vijana cha Miombo kilikidhi vigezo na kupata Mkopo wa Tsh. Mil 200. Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kikundi cha ‘Miombo Beekeeping Initiatives’ Bw. Edward Kitenyi amesema kwa sasa wameweza kufunga Mtambo wa kuchaka Asali na kwa mwezi mmoja wana uwezo wa kuzalisha Tani 1 ya Asali na wanasafirisha mpaka nje ya Mkoa wa Tabora.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad