Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango
akisalimiana na Mawaziri kutoka nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa
Ziwa Tanganyika wakati alipowasili katika Ukumbi wa Hoteli ya Lake
Tanganyika Mkoani Kigoma kwajili ya kufungua mkutano wa tisa wa
Mawaziri wa Nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango
akizungumza wakati wa ufunguzi mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi
wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika unaofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa hoteli ya lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Viongozi
mbalimbali wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani) wakati wa
ufunguzi mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Usimamizi
Endelevu wa Ziwa Tanganyika unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
hoteli ya lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango
akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wanaoshiriki Mkutano wa Tisa wa
Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika
mara baada ya kufungua mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa hoteli ya lake Tanganyika mkoani Kigoma. Desemba 16,2021. (
kutoka kushoto kwa Makamu wa Rais ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande, Waziri wa Uchumi wa Kijani na
Mazingira kutoka Zambia Mhe. Collins Nzovu, Waziri wa Mazingira , Kilimo
na Mifugo kutoka Burundi Mhe. Deo-Guide RUREMA na Waziri wa Uvuvi na
Mifugo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo Mhe. Adrien Bokele).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango
akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira wanaoshiriki mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi
wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika mara baada ya
kufungua mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya
lake Tanganyika mkoani Kigoma. Desemba
………………………………………………………….
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo
tarehe 16 desemba 2021 amefungua Mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi
wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika unaofanyika katika
Ukumbi wa Hoteli ya Lake Tanganyika mkoani Kigoma. Mkutano huo
unashirikisha Mawaziri wa Mazingira kutoka Tanzania, Burundi, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Zambia.
Akifungua
Mkutano huo Makamu wa Rais ametoa wito kwa nchi wanachama wa usimamizi
endelevu wa ziwa Tanganyika kushiriki kikamilifu katika kutoa michango
yao ya ushiriki ikiwemo ada ya mwaka ya uanachama huo ili kuwezesha
kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika uhifadhi
endelevu wa ziwa Tanganyika. Amesema Tanzania wakati wote ipo tayari
kikamilifu katika kushirikiana na nchi wanachama katika kutekeleza
mkataba wa usimamizi endelevu wa ziwa Tanganyika kwa maendeleo endelevu
ya ziwa hilo.
Aidha
Makamu wa Rais amesema ziwa Tanganyika limeendelea kuwa ziwa namba
mbili duniani kwa kina pamoja na uwingi wa maji huku likihudumia zaidi
ya watu milioni 10 wanaolizunguka ziwa hilo na kubarikiwa kuwa na
viumbe visivyopatikana mahali popote duniani hivyo mawaziri hao
wanapaswa kutafakari na kutoa njia zitakazowezesha ufuatiliaji wa
taratibu zilizowekwa katika nchi wanachama kukabiliana na uchafuzi wa
ziwa, uvuvi juu ya kiwango pamoja na mmomonyoko wa udongo.
Pia
amewataka mawaziri kutoka nchi wanachama wanaoshiriki mkutano wa tisa
wa usimamizi endelevu wa ziwa Tanganyika kutumia mkutano huo kama msingi
wa kuongeza makubaliano na ushirikiano na kuwezesha mamlaka ya
usimamizi ya ziwa Tanganyika kuongeza manufaa ya matumizi ya ziwa hilo
kwa vizazi vya sasa na baadae.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Hamad Hassan Chande amesema kuanzishwa kwa ushirikiano huo kulilenga
kubaini matishio na changamoto za uharibifu wa mazingira katika ziwa
Tanganyika ambapo mpaka sasa faida mbalimbali zimepatikana zikiwemo
kutekeleza kwa pamoja mpango wa maendeleo wa kanda wa ziwa Tanganyika,
kuandaa mkakati wa ulinzi wa Bioanuai na usimamizi endelevu wa maliasili
katika ziwa Tanganyika.
Naye
mwenyekiti wa mkutano huo Waziri wa Uchumi wa Kijani na Mazingira
kutoka Zambia Mhe. Collins Nzovu amesema ili kukabiliana na uharibifu wa
ziwa Tanganyika nchi wanachama zinapaswa kuweka mkazo katika maendeleo
ya kijani kwa kuweka sera kulinda mazingira wakati wa mipango ya
maendeleo ya kiuchumi pamoja na kupunguza uzalishaji gesi joto.
No comments:
Post a Comment