Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiwasilisha
ujumbe maalum wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, kwa Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri
anayeshughulikia masuala ya Rais wa Abu Dhabi, Mhe. Sheikh Mansour bin
Zayed Al Nanyan, mjini Abu Dhabi.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiwasilisha
ujumbe maalum wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, kwa Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri
anayeshughulikia masuala ya Rais wa Abu Dhabi, Mhe. Sheikh Mansour bin
Zayed Al Nanyan, mjini Abu Dhabi.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (katikati) akiwa
na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri anayeshughulikia masuala ya
Rais wa Abu Dhabi, Mhe. Sheikh Mansour bin Zayed Al Nanyan (kulia),
mjini Abu Dhabi, Falme ya Nchi za Kiarabu. Kushoto ni Waziri wa
Nchi-Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali,
Ikulu ya Abu Dhabi.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiagana na Naibu
Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Rais wa Abu
Dhabi, Mhe. Sheikh Mansour bin Zayed Al Nanyan (kulia), baada ya
kuhitimisha mazungumzo yao Ikulu mjini Abu Dhabi, Falme ya Nchi za
Kiarabu.
Ujumbe
wa Tanzania, ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameck Nchemba (wa tatu kushoto) ukiwa katika picha ya pamoja na Naibu
Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Rais wa Abu
Dhabi, Mhe. Sheikh Mansour bin Zayed Al Nanyan (katikati), baada ya
kuhitimisha mazungumzo yao, Ikulu, mjini Abu Dhabi, Falme ya Nchi za
Kiarabu.
Waziri
wa Nchi-Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali,
akiagana na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri anayeshughulikia
masuala ya Rais wa Abu Dhabi, Mhe. Sheikh Mansour bin Zayed Al Nanyan
(kulia), baada ya kuhitimisha mazungumzo yao, Ikulu, mjini Abu Dhabi,
Falme ya Nchi za Kiarabu.
Balozi
wa Tanzania katika Nchi za Falme za Kiarabu Mhe. Mohamed Mtonga,
akiagana na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri anayeshughulikia
masuala ya Rais wa Abu Dhabi, Mhe. Sheikh Mansour bin Zayed Al Nanyan
(kulia), baada ya kuhitimisha mazungumzo kati yake na ujumbe wa
Tanzania, Ikulu, mjini Abu Dhabi, Falme ya Nchi za Kiarabu.
Naibu
Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Rais wa
Abu Dhabi, Falme za Nchi za Kiarabu, Mhe. Sheikh Mansour bin Zayed Al
Nanyan (kulia), akimkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania
Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipowasili Ikulu ya Nchi hiyo
kuwasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
na kufanya nae mazungumzo, Ikulu, mjini Abu Dhabi.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Abu Dhabi)
……………………………………………….
Na Benny Mwaipaja, Abu Dhabi
SERIKALI
ya nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya Abu Dhabi imeahidi kuendeleza
ushirikiano katika masuala ya kiuchumi na kijamii na Serikali ya
Tanzania ili kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Ahadi hiyo
imetolewa mjini Abu Dhabi, Falme za Nchi za Kiarabu na Naibu Waziri Mkuu
ambaye pia ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Rais, Sheikh Mansour
bin Zayed Al Nanyan, baada ya kupokea ujumbe maalum kutoka kwa Mhe. Rais
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
uliowasilishwa kwake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameck Nchemba, Ikulu ya nchi hiyo.
Akizungumza baada ya
mazungumzo yao ya faragha, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameck Nchemba alisema kuwa Sheikh Mansour ameahidi kutuma ujumbe maalum
nchini Tanzania kwa ajili ya kuangalia miradi mbalimbali ya kimkakati
inayotokelezwa hivi sasa na mingine mipya kwa ajili ya kutoa fedha.
Dkt.
Nchemba aliitaja miradi iliyowasilishwa kwa Serikali ya Abu Dhabi kuwa
ni ile ya uendelezaji wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), mradi wa Ujenzi
wa Bwala la Kuzalisha Nishati ya Umeme wa Mwalimu Julius Nyerere,
ujenzi wa miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, kilimo na uvuvi
pamoja na elimu.
“Kwenye sekta ya elimu tumejenga madarasa mengi,
tumejenga vituo vya afya vingi sana na vingine viko vijijini lakini
hatujajenga nyumba za watoa huduma wanaotakiwa kufanyakazi kwenye maeneo
hayo” alisema Dkt. Nchemba.
Aidha, alisema kuwa wamejadiliana na
Mhe. Sheikh Mansour bin Zayed Al Nanyan kuhusu fursa za uwekezaji
zilizopo nchini zinazotokana na Tanzania kuwa lango la kibiashara kwa
nchi zisizozungukwa na bahari ambazo zikitumiwa vizuri kama vile uwepo
wa nishati ya mafuta na gesi, zitaifanya nchi ipae zaidi kiuchumi.
“Maeneo
mengine tuliyojadiliana ni namna ya kuitumia na kuishirikisha sekta
binafsi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa njia ya ubia kati ya
sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) ili kuleta faida kwa pande zote
mbili na wananchi kwa ujumla” aliongeza Dkt. Nchemba.
Kwa upande
wake, Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, alisema kuwa mkutano wao na
Naibu Waziri Mkuu wa Abu Dhabi uliangazia pia masuala ya Zanzibar ambapo
miradi kadhaa ya kimkakati inayotaka ufadhili iliwasilishwa.
Aliitaja
miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Manga Pwani kwa njia
ya ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi, Ujenzi wa nyumba za makazi za
gharama nafuu zipatazo 10,000 kwa ajili ya watumishi wa umma pamoja na
wananchi wengine na uchimbaji wa mafuta na gesi.
“Zanzibar tuna
fursa kubwa katika masuala ya uchumi wa blue ikiwemo uchimbaji wa mafuta
na gesi, masuala ya uvuvi na utalii na wenzetu wamepiga hatua kubwa
katika maeneo hayo, tukishirikiana nao katika maeneo hayo tutapiga hatua
kubwa kiuchumi na kijamii” alisema Mhe. Ali.
Aliishukuru Abu
Dhabi kwa kuendeleza ushirikiano na Tanzania hususan Visiwa vya Unguja
na Pemba ambapo nchi hiyo ya Kiarabu ilifadhili ujenzi wa Hospitali ya
Wete-Pemba na kwa kuahidi kuwa tayari kuendeleza ushirikiano huo katika
miradi mipya iliyowasilishwa kwao.
Friday, December 17, 2021

ABU DHABI YAAHIDI KUENDELEA KUIPIGA JEKI TANZANIA KIMAENDELEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment