JESHI Jeshi la Polisi limekamata jezi feki zinazouzwa zinazotumiwa na timu mbalimbali za hapa nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya
Polisi, David A. Misime - SACP amesema utengenezaji na uuzaji wa jezi
feki (zisizo na kiwango) ni kosa la jinai na kibaya zaidi wanaofanya
hivyo wanakuwa ukwepaji kulipa kodi kwa sababu hazipitii katika mfumo
ulio rasmi.
Misime
- SACP amesema baadhi ya timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu ya
Tanzania Bara, huingia mikataba na kampuni mbalimbali ya kutengeneza
jezi na pale zinapouzwa kiasi fulani huingia katika timu ili kugharamia
mahitaji ya wachezaji kama mishahara.
Amesema
Timu ya Polisi Tanzania imefanya hivyo kwa kuingia mkataba na baadhi ya
kampuni kama vile Lodhia Group of Companies na Kampuni ya Vunja Bei.
Kwa
bahati mbaya na kwa nia ovu ya kujipatia fedha kinyume cha sheria za
nchi, baada ya timu hizo kuingia mikataba, utengenezaji, usambazaji na
mauzo yanapo anza wapo watu wanaotengeneza jezi zilizo chini ya kiwango
(jezi feki) kwa kutumia nembo zilezile na kuanza kuziuza mitaani. Kwa
kufanya hivyo huinyima serikali mapato na kibaya zaidi timu hukosa
fedha zikiwepo za kuwalipa wachezaji.
amesema
msako ulioendeshwa na Jeshi la Polisi watuhumiwa 15 wameshakamatwa
kutoka maeneo ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Tabora na Tunduma ambapo
jumla ya Jezi feki 279, Urembo (ribons) 300 na Kofia 6 zimekamatwa.
Kesi zimefunguliwa dhidi yao na upelelezi ukikamilika watafikishwa
mahakamani.
Aidha
katika uchunguzi uliofanyika imebainika kuwepo na wafanyabiashara
waliofanya mawasiliano na viwanda vya ndani na nje ambavyo jezi halali
hutengenezwa wakitoa oda ya kutengenezewa jezi feki. Hawa nao ambao
jumla yao ni 11 wamefunguliwa jalada, wamehojiwa na ushahidi unaendelea
kukusanywa.
Amesema
Jeshi la Polisi Tanzania linatoa wito kwa watu wanaofanya hivyo kuacha
mara moja kwani watachukuliwa hatua endapo wataendelea kufanya uhalifu
huo.
Aidha
ametoa wito kwa timu ambazo zitabaini watu wanaotengeneza na kuuza jezi
feki zenye nembo walizokubaliana katika mikataba walioingia na kampuni
wasisite kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi ili hatua za kisheria
ziweze kuchukuliwa dhidi ya watu hao.
Pia
amewaasa Watanzania, wanapo nunua jezi za timu wanazozipenda na
kuzishabikia, wanunue kwenye maduka stahiki na pale watakapo baini
kuuziwa jezi feki wasisite kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi. Wananchi
tunaomba watambue jezi hizo feki wanauziwa bei ile ile ya jezi halali,
ambazo ukitumia hazidumu kama zile halali.
Tukumbuke
tatizo la bidhaa bandia (feki) ni la dunia nzima, tukilifumbia macho
hili la jezi feki wahalifu wana tabia ya kunogewa, watahamia hata katika
dawa za kutibu binadamu, mifugo na hata katika vifaa mbalimbali vya
matumizi ya binadamu na madhara yatakuwa kwetu sote.
No comments:
Post a Comment