Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza wakati
akifungua mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na
Washirika wa Maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi
Mkazi na Mratibu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti mwenza wa Washirika
wa Maendeleo Nchini Bw. Zlatan Milisic akizungumza wakati wa mkutano wa
Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo
uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es
Salaam.

Baadhi
ya Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali nchini na maafisa wa
Serikali wakifuatilia mawasilisho mbalimbali wakati wa mkutano wa
Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika Maendeleo
uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es
Salaam.

Baadhi
ya Wadau wa Maendeleo wakifuatilia mawasilisho mbalimbali katika
mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa
Maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
jijini Dar es Salaam.

Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba akisalimiana na
Mwakilishi Mkazi na Mratibu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti mwenza wa
Washirika wa Maendeleo Nchini Bw. Zlatan Milisic wakati wa mkutano wa
Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo
uliofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

Kamishna
wa Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Sauda Msemo
akifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano wa Majadiliano ya
Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika ukumbi wa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

Meza
kuu ikiwa katika picha ya Pamoja na washirika wa maendeleo walioshiriki
mkutano wa majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa
Maendeleo uliofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar
es Salaam.

Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza na
vyombo vya habari kando ya mkutano wa majadiliano ya Kimkakati kati ya
Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

Baadhi
ya wajumbe wa mkutano wa mazungumzo ya kimkakati kati ya Serikali na
washirika wa maendeleo wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano
huo uliohusisha washirika wa maendeleo, sekta binafsi pamoja asasi za
kiraia, uliofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es
Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini -WFM, Dar es Salaam)
*******************************
Na Saidina Msangi, Dar es Salaam
Serikali
imetoa wito kwa wadau wa maendeleo kuisaidia katika utekelezaji wa
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2021/22-2025/26
utakao gharimu jumla ya Sh. trilioni 114.9.
Wito
huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel
Tutuba alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili
wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo,
jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuwa mkutano huo utawezesha upatikanaji wa michango ya wadau ili
kuboresha sera na miongozo mbalimbali ili kuwezesha utekelezaji wa
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano pamoja na
maandalizi ya mwongozo wa uandaaji wa mipango na bajeti ya Serikali kwa
mwaka 2022/23.
“Mkutano
hu utatoa fursa kwa Wadau wa Maendeleo kuona maeneo wanayoweza
kuchangia hasa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka
Mitano katika miradi wanayoweza kuchangia,”alisema Bw. Tutaba.
Alitoa
wito kwa wadau wa maendeleo wanaochangia katika utekelezaji wa miradi
mbalimbali nchini kutoa ahadi zao mapema katika kuchangia bajeti ya
Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 ili kuiwezesha Serikali kuandaa
bajeti halisi.
Alisema
maandalizi ya bajeti yatatokana na mazungumzo ya mkutano huo ambapo
sekta mbalimbali zinatarajiwa kuwasilisha zilivyojiandaa katika taasisi
zao, changamoto zilizojitokeza na mapendekezo ambayo Serikali
itayaingiza kwenye bajeti.
Alisema
Serikali inaendelea kujenga mazingira wezeshi ikiwemo sera imara,
kupunguza urasimu kuvutia sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika
utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa kuchangia kiasi
cha Sh. trilioni 40.6 na Serikali kuchangia kiasi cha Sh. trilioni 74.3.
“Tunakaribisha
sekta binafsi kushiriki katika miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo
utekelezaji wa miradi iliyoainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo
wa Taifa, mradi wa ujenzi wa reli ya mwendo kasi pamoja na kuimarisha
utendaji wa Shirika la Ndege nchini-ATCL ,”alisema Bw. Tutuba.
Aidha,
Bw. Tutuba alizielekeza taasisi za elimu na utafiti nchini kufanya
tafiti zitakazoiwezesha Serikali kuboresha utoaji wa huduma na hasa
maeneo yanayoweza kuibua vyanzo vipya vya kodi ili kuchangia bajeti ya
Serikali.
Mkutano
huo wa siku mbili uliohudhuriwa na makatibu wakuu, wadau wa maendeleo,
asasi za kiraia, sekta binafsi pamoja na maafisa wa serikali nchini kwa
mara ya kwanza umeshirikisha asasi za kiraia na Sekta Binafsi kutokana
na mchango wake mkubwa katika maendeleo nchini.
Kwa
upande wake Mwakilishi Mkazi na Mratibu wa Umoja wa Mataifa na
Mwenyekiti mwenza wa Washirika wa Maendeleo Nchini Bw. Zlatan Milisic
ameipongeza Serikali kwa hatua mbalimbali za kuleta mageuzi ya kijamii
na kiuchumi nchini.
Bw.
Milisic amepongeza hatua ya Serikali kuruhusu wanafunzi wanaopata
ujauzito kuruhusiwa kurudi shuleni kuendelea na masomo kwa mfumo wa
kawaida na kuahidi kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali
katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa Sekta ya Binafsi Nchini
Bw. Andrew Mahiga alisema kuwa Sekta binafsi nchini iko tayari
kushirikiana na Serikali kutekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa
na kuwa itachangia kuwekeza katika sekta za kilimo, mifugo, Tehama na
uchumi wa bluu kwa kuwekeza na kushauri masuala ya sera ili kufikia
malengo yaliyopangwa na Serikali.
Bw.
Mahiga ameishukuru Serikali kwa kuijumuisha sekta binafsi katika
mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya nchi na namna inavyoendelea
kuishirikisha katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo na
kupokea maoni yao.
No comments:
Post a Comment