MOUNT HANANG' QUEENS YAIBUGIZA GITTING VETERANS MABAO 2-0 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 22, 2021

MOUNT HANANG' QUEENS YAIBUGIZA GITTING VETERANS MABAO 2-0

 


Na Mwandishi wetu, Hanang'


TIMU ya soka la wanawake ya daraja la kwanza ya Mount Hanang' Queens ya Wilayani Hanang' Mkoani Manyara, imeibugiza mabao 2-0 timu ya Gitting Veterans.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Gitting juzi mabao ya timu hiyo yalipatikana kwenye kila kipindi.

Mshambuliaji wa timu hiyo Agnes Chuwa alifunga bao la kwanza dakika ya 17 kwa kichwa baada ya kona iliyopigwa na kiungo mshambuliaji Fatuma Yassin.

Kiungo mkabaji Rachel Samwel ameipatia bao la pili timu hiyo kwenye dakika ya 55 ya mchezo huo, baada kumalizia shuti kali la kiungo mshambuliaji Fatuma Yassin.

Mdhamini wa timu hiyo Paul Phares Mnyandwa amesema ataipeleka timu hiyo wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa ajili ya kucheza michezo ya kirafiki.

Mwenyekiti wa timu hiyo mwalimu Gisella Msofe amesema timu hiyo ya daraja

la kwanza inaendelea na mapambano hadi ipande ligi kuu.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Robert Massay amesema Mount Hanang' Queens ina uwezo mkubwa na inaweza wa kushinda timu kubwa za Simba Queens na Fountain.
1 comment:

Post Bottom Ad