WAZIRI NDUMBARO AZIONGEZEA MUDA WA KUFANYA KAZI BODI YA WAKURUGENZI YA Taff na TAWA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 24, 2021

WAZIRI NDUMBARO AZIONGEZEA MUDA WA KUFANYA KAZI BODI YA WAKURUGENZI YA Taff na TAWA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akikabidhiwa taarifa ya utendaji wa kipindi cha miaka mitatu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania ( Taff) Prof.Romanus Ishengoma ambapo Bodi hiyo imeongezewa muda wa kuendelea kutekeleza majukumu yake kisheria hadi pale itakapotangazwa Bodi mpya katika makabidhiano yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akikabidhiwa taarifa ya utendaji wa kipindi cha miaka mitatu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wantamapori Tanzania ( TAWA) Meja Jenerali Hamisi Semfuko ( kulia) ambapo Bodi hiyo imeongezewa muda wa kuendelea kutekeleza majukumu yake kisheria hadi pale itakapotangazwa Bodi mpya katika makabidhiano yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania ( Taff) mara baada ya kumalizika kikao cha kukabidhi taarifa ya utendaji wa kipindi cha miaka mitatu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania ( Taff) Prof.Romanus Ishengoma ( wa pili kulia)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( kulia) akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Misitu Tanzania (Taff) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Godwin Gondwe mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bodi ya Taff kilichofanyika leo Jijini Dodoma ambapo Waziri Ndumbaro ameiongezea Bodi hiyo muda wa kuendelea kufanya kazi.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) mara baada ta kumaliza kikao kilichofanyika leo Jijni Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Meja Jenerali ( Mst) Hamisi Semfuko
 
 ======   ======   ====

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameongeza  muda wa kuendelea kufanya kazi kisheria kwa  Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania ( TAFF) pamoja na Bodi ya Wakurugenzi  ya Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) ambazo muda wake wa kufanya kazi ulikuwa unaishia tarehe 25 Oktoba mwaka huu.

Ametoa uamuzi huo mapema leo Jijini Dodoma kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akikabidhiwa taarifa ya  utendaji wa kipindi cha miaka mitatu na Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi wa Bodi hizo wakiwa wameambatana na Wajumbe wao.

Dkt.Ndumbaro amewaeleza Wajumbe wa Bodi hizo kuwa wataendelea kutekeleza majukumu yao kisheria katika Taasisi hizo hadi pale atakapotangaza Bodi mpya huku akitaja moja ya sababu iliyomfanya kuchukua uamuzi kuwa ni kuridhishwa na utendaji kazi wa Bodi zote mbili.


" Uamuzi huu nimeufanya baada ya kujiridhisha katika kipindi chenu cha miaka mitatu mmefanya kazi nzuri na kwa ushirikiano sijaona sababu ninyi kuishia leo kufanya kazi zenu nawapongezeni sana" amesisitiza Dkt.Ndumbaro

Hata hivyo, Dkt.Ndumbaro licha ya kuongeza muda wa kufanya kazi  kwa Bodi hizo hakuweza kutaja muda maalumu ambao Bodi hizo  zitahudumu  licha ya kusisitiza kuwa muda wa Bodi ya TAWA na Taff utakoma  hadi pale tu atakapotangaza Bodi mpya.

" Ninaweza nikatangaza Bodi mpya  hata kesho au nisitangaze Bodi hizo  kwa kipindi cha miaka mitatu ninachosisitiza kipindi chenu kitaisha pale tu nitakapotangaza Bodi mpya" amesisitiza Dkt.Ndumbaro.

Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro ameitaka Bodi ya TAWA kuhakikisha inaisimamia taasisi hiyo ipasavyo kwa kuhakikisha  inaendeshwa kibiashara na sio kama ilivyo sasa ambapo utendaji kazi wake wa kushughulikia changamoto za Wawekezaji umekuwa ni wa taratibu sana hali inayowakazwa Wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika maeneo wanayoyasimamia

Kwa upande wa Bodi ya Wadhamini wa Taff, Dkt.Ndumbaro ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha inakuja na suluhisho ya kuhakikisha fedha inazozitoa katika Halmashauri nchini kwa ajili ya kuanzisha viwanda vya kuchakata asali zinasimamiwa ipasavyo huku akitaka viwanda vya kuchakata asali vinavyoanzishwa kwenye baadhi ya Halmashauri  vinakuwa endelevu kwa kushirikisha Sekta binafsi katika  uendeshaji wake

Aidha, Dkt.Ndumbaro amezitaka Bodi hizo kutokusita kuwachukulia hatua Watumishi wote ambao wapo chini ya mamlaka yao  watakaobainika kwenda kinyume na maadili ya utendaji kazi na kusisitiza kuwa  wale ambao hawana mamlaka nao watoe taarifa Wizarani na yeye kama Waziri nwenye dhamana na Wizara hiyo hatosita kuchukua hatua sitahiki kwa watakaokwenda kinyume na taratibu za kijeshi

" Nataka mkafanye kazi yule atakayetaka kutoboa mtumbwi tukimbaini tutamvisha mawe na kumtosa majini ili atuache sisi tuendelee na safari yetu" amesisitiza Dkt.Ndumbaro

Kwa upande wao Wenyeviti wa Bodi hao Meja Jenerali  (Mst.) Hamisi Semfuko wa TAWA pamoja Prof. Romanus Ishengoma wa Taff wamemshuku Waziri Ndumbaro kwa imani kubwa aliyoionesha kwao na kuahidi kuwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa maslahi mapana ya Taasisi hizo na kwa niaba ya Watanzania wote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad