HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 24, 2021

Rais Ndayishimiye wa Burundi apongeza Benki ya CRDB

BENKI ya CRDB imepongezwa kwa kufanikisha kuimalika kwa ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzaniana Burundi kupitia huduma zake za kibenki.

Akizungumza jijini Dodoma siku ya Ijumaa baada ya kuweka jiwe la msingi la uijenzi wa kiwanda cha Itracom Fertilizers Limited cha wawekezaji kutoka Burundi, Rais Evariste Ndayishimiye alisema, benki ya CRDB imekuwa mshirika mkubwa wa kuimalisha biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili. Benki ya CRDB imetoa mkopo wa kuwezesha ujenzi wa kiwanda hicho cha mbolea.
 
“Uwezeshaji uliofanywa na benki katika ujenzi wa kiwanda hiki cha mbolea ni ushahidi tosha wa namna gani benki imejikitia katika kufanikisha kuimalika kwa biashara na uwekezaji baina ya nchi zetu zenye udugu wa karibu,” Rais Ndayishimiye alisema.
Alisema uwekezaji huo wa raia kutoka nchini kwake, utawezesha kiwanda cha mbolea cha Itracom kuzalisha tani laki sita kwa mwaka na kutoa ajira kwa Watanzania wasiopungua elfu 10.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki yake yenye matawi matatu nchini Burundi imekuwa ikitoa mikopo kwa miradi mbali mbali ya kimkakati ya serikali ya Burundi na Tanzania. Benki inatarajia kufungua tawi la nne wilayani Gitega mwaka huu.
Nsekela alisema benki yake imekuwa inafanya biashara kwa muda mrefu na wawekezaji wa Itracom huko Burundi kwa kuwapatia huduma zote za kibenki. Miongoni mwa miradi ambayo benki imefadhili huko Burundi ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha mbolea cha Fomi na kiwanda cha simenti huko Rutana ambacho benki imetoa mkopo wa dola za Marekani milioni 10.

“Mheshimiwa Rais, umepo wako hapa leo kuweka jiwe la msingi kwaajili ya ujenzi wa kiwanda cha Itracom ni ushahidi tosha wa kuimalika kwa uhusiano baina ya Burundi na Tanzania. Kama benki ya kizalendo yenye mtazamo wa kimataifa, Benki ya CRDB ina mkakati wa maksudi wa kuwezesha kuimalika kwa mahusiano ya kibiashara na uwekezaji baina ya nchi za Afrika ya Mashariki ili kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watu,” alisema.
Mkurugenzi huyo wa Benki ya CRDB aliongeza kwamba benki hiyo imeshawekeza mtaji wa kiasi cha dola 107 milioni nchini Burundi katika sekta mbalimbali za uchumi wan chi hiyo ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa maji Mpanda.

Benki hiyo pia imewezesha kampuni ya Itracom kuwekeza katika kiwanda cha mbolea cha Minjingu kilichopo Babati mkoani Manyara. “Hapa nchini Tanzania benki yetu imewezesha kampuni ya Itracom kwa kuipatia mkopo wa dola 12 milion kwaajili ya ujenzi wa kiwanda cha Minjingu kilichopo Babati,” Nsekela alisema.
Tangu ianzishe kampuni tanzu nchini Burundi mwaka 2011, Benki ya CRDB imetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa kupitia kutoa ajira kwa Warundi na pia kulipa kodi mbalimbali za serikali kufanikisha maendeleo.


 










 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad