HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 15, 2021

TAKUKURU IRINGA WATOA ELIMU YA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA WANANCHI

Afisa TAKUKURU wilaya ya Iringa Aneth Mwakatobe akisikilizwa na baadhi ya wananchi wakati akitoa elimu ya kupambana na rushwa.
Afisa TAKUKURU wilaya ya Iringa Aneth Mwakatobe akiwa kwenye moja ya mikutano ya hadhara ambayo alikuwa akitoa elimu juu ya kupambana na rushwa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) wilaya ya Iringa imewataka wananchi kutoa taarifa za miradi ambayo inatekelezwa chini ya kiwango ukilinganisha na thamani ya fedha ambazo serikali imetoa na kuwataka kuacha tabia ya kutoa na kupokea rushwa kwa kufanya hivyo kunarudisha nyuma shughuli za kimaendeleo kwa taifa na watu binafsi.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara ya mkuu wa wilaya ya Iringa ya kusikiliza kero za wananchi,Afisa TAKUKURU wilaya ya Iringa Aneth Mwakatobe alisema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kuzilinda rasilimali za nchi kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa wananchi wamekuwa wakiwashawishi baadhi ya viongozi kutoa rushwa kwa ajili ya kufanikisha malengo ya kinyume na taratibu ambazo zinatakiwa na wananchi wanaongoza kwa kuombwa rushwa na baadhi ya viongozi hivyo kufanya kitendo hicho ni kosa kubwa katika kukuza maendeleo ya nchi.

“Kuna wakati wananchi wanatoa zawadi kwa viongozi kwa lengo la kufanikisha jambo furani bila kiongozi bila kujua hivyo sio dhambi kutoa zawadi kwa viongozi ila inakuwa dhambi unapotoa zawadi hiyo kwa malengo yako ambayo yanakuwa kinyume na sheria za nchi” alisema Mwakatobe

Mwakatobe alisema kuwa taasisi ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) inaangalia sana makosa yanayotokana na rushwa katika jamii kwa kuwa makosa ya rushwa yapo kila kona ya jamii hasa katika maeneo ambayo jamii inapata au inatoa huduma za kijamii.

Alisema kuwa serikali imekuwa inatoa fedha nyingi za kimaendeleo zinaenda kufanya kazi kwenye vijiji na mitaa ambayo kwa kiasi kikubwa inawalenga wananchi wa maeneo husika hivyo kila mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa miradi ambayo inatekelezwa kwenye maeneo yao kwa kuwa miradi hiyo ni mara ya wananchi.

“Miradi yote inayoletwa kwenye maeneo yenu ni mali yenu hivyo mnapaswa kuilinda na kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kulingana na thamani ya fedha ambayo inakuwa imetolewa na serilikali kwenye mradi husika” alisema Mwakatobe

Mwakatobe alisema kuwa bila kuisimamia vilivyo miradi hiyo basi serikali itakuwa inapoteza fedha nyingi bila mafanikio yanayotarajiwa hivyo wananchi wanajukumu la kuhakikisha wanasimamia jukumu hilo kikamilifu ili miradi itekelezwe kama inavyotakiwa.

Aliwaomba wananchi wa wialaya ya Iringa kutoa taarifa pale ambapo wanahisi kunaharufu ya rushwa kwa kupiga bure namba ya simu ya 113 ambayo itawasaidia taasisi hiyo kupata taarifa hizo na kuanza kuzifanyia kazi mara moja.

Alimazia kwa kuwataka wananchi kuikata rushwa kwa kuacha tabia ya kutoa rushwa,kuwashawishika kupokea rushwa hapo ndio Tanzania itapata maendeleo yanayotakiwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad