HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 16, 2021

NAIBU WAZIRI KASEKENYA AFUNGUA KIKAO CHA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA WIZARA NA TAASISI ZILIZOPO CHINI YA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI

Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya amefungua kikao cha 14 cha wadau wa sekta ya ujenzi na  uchukuzi  cha tathmini ya  utekelezaji wa shughuli za Wizara  (14th Annual Joint Transport sector review-JTSR 2021)  kilichofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Oktoba 15, 2021.

Katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza. S. Johari amewasilisha taarifa ya  utekelezaji wa shughuli za Mamlaka  na kusisitiza kwamba mbali na changamoto za ugonjwa wa UVIKO-19, Mamlaka imeendelea kutekeleza miradi yake. Ameeleza kuwa sekta ya usafiri wa anga inaanza kuimarika kutokana na idadi ya abiria na miruko ya ndege kuongezeka.

Pia, Bw. Johari ametumia fursa hiyo kuelezea mpango mkakati wa kuanzisha chuo cha kisasa cha usafiri wa anga ukanda wa Afrika mashariki ambapo hatua za awali ikiwa ni pamoja na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa chuo hicho zimeshafanyika 

Kikao hicho cha siku moja kimeandaliwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambapo Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo pamoja na wadau wa maendeleo wameshiriki kikamilifu.

 Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akifungua kikao cha pamoja cha kutathmini utekelezaji wa shughuli za Wizara na taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo -JNICC Oktoba 15, 2021.
Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza na wakuu wa taasisi zilizopo chini ya Wizara pamoja na wadau wa maendeleo wakati wa kikao cha  pamoja cha kutathmini utekelezaji wa shughuli za Wizara hiyo (14th Annual Joint Transport sector review-JTSR 2021)  kilichofanyika ukumbi wa JNICC Oktoba 15, 2021.
Mkurugenzi Mkuu TCAA, Hamza S. Johari  pamoja  na Mkurugenzi Mkuu TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakifuatilia mada wakati wa kikao hicho katika ukumbi wa JNICC Oktoba 15, 2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka wakati wa kikao cha pamoja kilichoandaliwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Oktoba 15, 2021.
Picha ya Pamoja
Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya akiweka sahihi alipowasili kwenye banda la Chuo Cha Usafiri wa Anga (CATC) kilichopo chini ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Kulia ni Bw. Hamza Johari- Mkurugenzi Mkuu TCAA.
Mkuu wa Chuo Cha Usafiri wa Anga (CATC) Bw. Aristid Kanje akielezea mpango mkakati wa Ujenzi wa Chuo Cha Usafiri wa Anga kwa Naibu Waziri Mhandisi Kasekenya alipotembelea banda la Chuo hicho  katika ukumbi wa JNICC Oktoba 10, 2021.
Meneja Rasilimali Majengo TCAA, Swalehe Nyenye akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya alipotembelea banda la Chuo cha Usafiri wa Anga CATC katika ukumbi wa JNICC


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad