HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 16, 2021

TMA YAPONGEZWA KWA KUTOA UTABIRI WENYE TIJA NCHINI


Dk. Kijazi akipata maelezo kutoka wadau wanufaika wa huduma za Utabiri za TMA kwenye mkutano huo.  

Mtaalam wa Hali ya Hewa toka TMA, Abubakar Lungo (kushoto) akimweleza mgeni rasmi na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (kulia) namna TMA inavyofanya kazi na wadau walioshiriki Mkutano wa 14 wa sekta ya Uchukuzi wenye lengo la kupima utendaji wa sekta mbalimbali za uchukuzi. Katikati ni Mkurugenzi wa Tehama na huduma za ufundi, Dr. Pascal Waniha akifuatilia.

Mkurugenzi wa Tehama na huduma za ufundi, Dr. Pascal Waniha (kulia) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya mara baada ya kutembelea Banda la TMA kwenye Mkutano wa 14 wa sekta ya Uchukuzi uliokuwa na lengo la kupima utendaji wa sekta mbalimbali za uchukuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Tehama na huduma za ufundi, Dr. Pascal Waniha (kulia) kwenye Banda la TMA waliposhiriki Mkutano wa 14 wa sekta ya Uchukuzi uliokuwa na lengo la kupima utendaji wa sekta mbalimbali za uchukuzi.
Mgeni rasmi na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (mwenye suti nyeusi) akisikiliza maelezo ya juu ya utendaji kazi wa TMA kutoka kwa Mkurugenzi wa Tehama na Huduma za ufundi, Dr Pascal Waniha alipotembelea banda la TMA wakati wa Mkutano wa 14 wa sekta ya Uchukuzi wenye lengo la kupima utendaji wa sekta mbali mbali za uchukuzi alipotembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Na Karama Kenyunko Michuzi TV 
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kuendelea kutoa taarifa za Hali ya Hewa zinazosaidia sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya usafirishaji wa ardhini na majini pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara.

Mhandisi Kasekenya amesema hayo leo Oktoba 15, ijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano wa 14 wa sekta ya Uchukuzi wenye lengo la kupima utendaji wa kazi wa sekta mbalimbali za uchukuzi.

Amesema,katika nchi za Afrika TMA ni miongoni mwa Taasisi inayofanya kazi bora zaidi kuliko nyingine kutokana na kutoa taarifa zinazosaidia sekta mbalimbali nchini kwa kutoa Utabiri wa Hali ya hewa kwa nchi  nyingi ambazo zimekuwa zikiizunguka Tanzania na hivyo kuepuka majanga 

Mhandisi Kasekenya amesema TMA ni Taasisi muhimu ambayo imekuwa ikisaidia sekta zote katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati hususani ya barabara kufahamu taarifa za hali ya hewa kwa yanayotarajiwa kutokea na kwa wakati gani namkiweza kuepusha madhara mbali mbali yanayoweza kutokea kutokana mabadiriko ya hali ya hewa

"Ni vema katika ujenzi wa miradi yeyote kuhakikisha unafatwa utaratibu wa kitaalamu wa kufahamu mazingira hayo ili kuweza kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza" amesema Mhandisi Kasekenya.

Akitolea mfano namna utabiri wa hali ya hewa unavyosaidia, amesema hata naodha wa meli anapoendesha chombo hicho ni lazima kwanza ajue na apate taarifa kutoka TMA ndipo afanye kazi yake.

Akizungumza kuhusu mkutano huo Mhandisi Kasekenya amesema kila mwaka kumekuwa kukifanyika mkutano huo lengo kuu likiwa ni kufanya tathimini ya kazi mbalimbali ambazo zinafanyika katika sekta nzima ya Uchukuzi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt Agness Kijazi amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikitumika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo,  sekta ya uchukuzi ikiwemo Anga, Reli,masuala ya barabara,na miradi mikubwa ya ujenzi hata bwawa la Nyerere ambalo linaendelea na ujenzi.

amesema TMA inatambua kuwa Shughuli za Uchukuzi nyingi zinaendana zaidi na masuala ya Utabiri wa Hali ya hewa na ndio maana katika maonesho hayo wameonyesha ni huduma gani wanazozitoa na kuwaonyesha jinsi  utabiri unavyotolewa na namna unavyotumika kwani ni muhimu katika sekta hizo na hasa katika kipindi  ambacho kuna mabadiliko ya tabia ya nchi duniani.

Aidha Dkt Kijazi ameziasa taasisi mbalimbali kuangalia masuala ya hali ya hewa kabla ya kuanza kufanyika kwa mradi mkubwa ili kuepuka kuuweka mradi huo kwenye hatari ya kuharibika pindi litakapotoke na kulazimika kufuta ili kuja kuanza upya.

Katika mkutano huo Taasisi mbalimbali zikiwemo za serikali na sekta binafsi za usafirishaji wa ardhini na majini zimeweza kushiriki kwa kujadili utendaji kazi katika ufanyaji wa Shughuli zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad