HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 15, 2021

MAHAFALI YA SHULE YA SEKONDARI MAGOZA YAFANA, MKURUGENZI KITAAMBA CHEUPE ATOA MSAADA


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kitambaa Cheupe Microfinance Limited, Jessica kikumbi akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Magoza yaliyofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dar es Salaam.Na Avila Kakingo, Blog ya Jamii
MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya Kitambaa Cheupe Microfinance Limited, Jessica kikumbi ametoa msaada Kompyuta, Printer na pedi kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Magonza iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam.

Msaada huo ameutoa wakati wa mahafali ya 12 ya shule ya Sekondari Magonza Oktoba 15, 2021.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo Jessica alisema kuwa aliona Changamoto za shule hiyo kwa walimu wakati wa kuprint (Kuchapisha) mitihani ya shule.

"Nimesikiliza Risala yao na nikaona uwezo ninao wa kusaidia, ambapo nimetoa Kompyuta, Printer na Pedi kwaajili ya watoto wa kike wapatapo dharula wawapo shuleni. Nimeona niwarahisishie watoto wakike kuja shule wakati kipindi wakiwa katika kipindi cha Hedhi." Amesema Jessica

Hata hivyo Jessica amewashauri watoto wakike pamoja na wakiume katika shule hiyo kujiadhari na mitandao au ukuaji wa teknolojia kwani kwa kipindi ambacho teknolojia imekuwa kumekuwa na ukatili wa kingono unaofanyika mitandaoni.

Ametoa mfano wa Mtandao wa kijamii wa BBC Swahili kuwa ulilipoti kuwa katuni za watoto ya Supper Man itakuwa ikihamasisha Mapenzi ya jinsia moja hivyo wazazi wameaswa kuwa makini na hilo kwani Teknolojia itazalisha kizazi ambacho si cha Kawaida.

"Nimewasisitizia wazazi wanafunzi wajiepushe na mambo ya mtandao na wawe makini wachague nini cha kukiangalia na wanachokifata mtandaoni, wazazi wasiwaachie watoto simu bila kujali ni nini mtoto anakiangalia mtandaoni na kwenye vipindi vya Mtandaoni, wazazi ili kukiokoa kizazi hiki ni wazazi kuwalinda wazazi na mitandao inayofundisha maovu." Amesema Jessica

Amesema kuwa wazazi wanajukumu la kukiokoa kizazi hiki na unyanyasaji wa kingono kimtandao ambapo kwa sasa asilimia kubwa unyanyasaji huo umeanza kutamalaki hapa nchini.

Takwimu zinaonesha Watoto wa shule za sekondari kidato cha kwanza (1) hadi kidato cha nne (4); takriban watoto wa 5 Kati ya 10 wanamiliki Simu, wengine wanamiliki line za Simu, Saba (7) Kati ya 10 wanatumia Simu nyumbani; na watano (5) Kati ya 10 wamejiunga kwenye mitandao ya kijamii; nane (8) Kati ya 10 wanatumia Internet.

Kuhusu athari sita (6) Kati ya 10 wamenyanyaswa kwenye mitandao; wanne (4) Kati ya 10 wamewanyanyasa wenzao kwenye mitandao.

Hata hivyo Jessica amewaasa jamii wanaotaka kutoa msaada au kurudisha katika jamii watoe katika sekta ya elimu kwani elimu ndio ufunguo wa Maisha.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Magonza, Kalunde sigera amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kitambaa Cheupe Microfinance Limited, Jessica kwa kutoa msaada huo.

"Tunamshukuru sana Mgeni Rasmi wetu wa Mahafali ya 12 ya Shule ya Sekondari ya Magonza kwa kutoa msaada huu utasaidia walimu katika kuchapa mitihani katika shule hiyo na pedi zitasaidia kwa wanafunzi wakike wapata Hedhi ya zalula wawapo shuleni."

Licha ya hayo Mkuu wa shule huyo ameomba jamii inayoweza kusaidia shule ya Msingi Magoza kusaidia kujenga ukuta wa kuzunguka shule pamoja na ujenzi wa geti, pia kusaidia kutengeneza mfumo wa uchakataji wa Takataka, Vifaa vya kuhifadhia Maji hasa uvunaji maji ya mvua yatakayosaidia kumwagilia maua katika shule hiyo.

Hata hivyo Mkuu wa shule huyo amesema kuwa wanaomba jamii iwasaidie kupata kifaa kinachoweza kubadili maji chumvi na kuwa maji baridi yasiyokuwa na chumvi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kitambaa Cheupe Microfinance Limited, Jessica kikumbi akikabidhi boksi la pedi kwaajili ya wanafunzi wakike katika shule ya Sekondari ya Magonza iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya 12 ya shule hiyo yaliyofanyika Oktoba 14,2021.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kitambaa Cheupe Microfinance Limited, Jessica kikumbi akikata keki katika maafali ya 12 ya shule ya sekondari Magoza iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam Oktaba 14,2021.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Magonza, Kalunde sigera akizungumza wakati wa Mahafali ya 12 ya shule ya Sekondari ya Magoza liyofanyika Oktoba 14,2021 Tabata jijini Dar es Salaam.














Wazazi na walezi wakiwa katika mahafali ya 12 ya shule ya sekondari Magoza iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam.


Wanafunzi wa shule ya Sekondari Magoza iliyopo Tabata jijini Dar Es Salaam wakiwa katika Mahafali ya 21 ya shule hiyo.
Meza kuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad