HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 28, 2021

RAIS WA ZANZIBAR DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AHUTUBIA MAADHIMISHO YA MIAKA 76 YA UN UKUMBI WA SHEIKH IDRISA ABDULWAKIL KIKWAJUNI ZANZIBAR

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bw. Zlatan Milisic,Mratibu wa UN Zanzibar.Bi.Dorothy Temu Usiri na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui, alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, kuhutubia maadhimisho ya miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Afisa wa WHO .Dr.Vendeun Simon alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya Vijana wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa (UN) na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar.Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea mabanda ya maonesho ya Vijana ya kuadhimisha Miaka 76 ya UN, yaliofanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw.Zlatan Milisic na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar.Mhe.Nassor Ahmed Mazrui.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mmoja wa Vijana walioshinda Shindano la Ubunifu Barke Abdullah Ukusi.(hayupo pichani) akielezea Ubunifu wake wa Samaki Mtandaoni, wakati wa hafla ya kuadhimisha Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN, yalioadhimisha Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw.Zlatan Milisic na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui.
MKURUGENZI wa SMIDA Bw. Soud Said Ali akitowa maelezo kuhusiana na Shindano la Kibunifu kwa Vijana Wajasiriamali kuhusiana na Uchumi wa Buluu, wakati wa kuwazawadia washindi wa shindano hilo sambamba na Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
BAADHI ya Vijana na Wageni waalikwa katika  Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa, wakifuatilia hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
MBUNIFU Kipimo cha Ujazo wa Mafuta katika Matenki ya Kuhifadhia Mafuta (Computerised System for Oil Measuring) Ndg. Hamid Abdullah Wailu, akitowa maelezo ya ubunifu wake huo wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN, yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
MRATIBU Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw. Zlatan  Milisic akizungumza na kutowa maelezo ya Maadhimisho ya Umoja wa Mataifa kutimiza Miaka 76 tangu kuazishwa kwake, hafla hiyo ya maadhimisho imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
BAADHI ya Mabalozi Wadogo wanaofanytia Kazi zao Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN, katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi, hafla iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mmoja wa Vijana walioshinda Shindano la Ubunifu Barke Abdullah Ukusi.(hayupo pichani) akielezea Ubunifu wake wa Samaki Mtandaoni, wakati wa hafla ya kuadhimisha Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN, yalioadhimisha Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw.Zlatan Milisic.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Husseinn Ali Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti na fedha Mshindi wa Shindano la Ubunifu kwa Vijana Wajasiriamali Barke Abdaalah Ukusi kwa Ubunifu wake wa Samaki Mtandaoni na (kushoto kwa Rais) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw. Zlatan Milisic na (kuia kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti na fedha Mshindi wa Shindano la Ubunifu kwa Vijana Wajasiriamali Mohammed Wanimo kwa Ubunifu wake wa Mashine ya Kusagia Mwani na (kushoto kwa Rais) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw. Zlatan Milisic na (kuia kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad