HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 21, 2021

Njombe:Sekretarieti ya CCM yamuagiza mkurugenzi Makambako kusaidia ujenzi wa ofisi ya kata

 Na Amiri Kilagalila,Njombe

SEKRETARIETI ya Chama Chama Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe imemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Makambako kuwaunga mkono wananchi katika ujenzi wa ofisi ya kata ya Lyamkena ambayo imegharimu zaidi ya Milioni 48 mpaka sasa.

Agizo hilo limetolewa na katibu wa CCM Mkoa Bi Amina Imbo mara baada ya Sekretarieti ya chama hicho kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ofisi hiyo ya kata ya Lyamkena iliyojengwa kwa nguvu za wananchi,Mhe.Diwani wa viti maalumu anayetoka katika kata hiyo, Mhe.Diwani wa kata hiyo na Mhe.Mbunge wa Jimbo la Makambako Deo Sanga.

Katika ziara hiyo Sekretarieti imetoa maelekezo kwa Viongozi wa Wilaya,kata,Matawi na Mashina kusajili wanachama wapya katika mfumo wa kieletroniki na kusisitiza kuendelea kuingiza wanachama wapya sambamba na ulipaji wa ada za uanachama kwa kuwa kushindwa kutekeleza agizo hilo ni tafsiri viongozi hao kukosa sifa za kugombea katika nafasi zao katika uchaguzi wa Chama mwaka 2022.

Vile vile lengo jingine la ziara hiyo imekuwa ni muendelezo wa kuimarisha uhai wa chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya shina kwa kuwa ndiko wanachama wa CCM waliko,kupitia hilo Sekretarieti ya Mkoa imeshiriki kikao cha Mwenyekiti wa Shina katika kata ya Makambako tawi la Ubena katika shina namba Moja la tawi hilo, na kupitia ushiriki huo Katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Njombe amewataka mabalozi wengine kujenga utamaduni wa kufanya vikao na wanachama wao mara kwa mara ili kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya Chini.

Katika ziara hiyo katibu wa CCM mkoa ameongozana na katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Njombe Cde,Erasto G.Ngole Cde,Amosi Kusakula katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe,Bi Frola Kapalia Katibu wa U.W.T Mkoa wa Njombe pamoja na Bi,Agatha Lubuva katibu wa wazazi mkoa wa Njombe.
Katibu wa CCM Mkoa Bi Amina Imbo akizungumza na sekretariel ya CCM Makambako Mkoani Njombe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad