HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 25, 2021

MKUU WA MKOA WA RUKWA ASISITIZA ELIMU YA KODI KWA WAFANYABIASHARA MKOANI RUKWA

 MKUUMkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Joseph Mkirikiti ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuendeleza utoaji elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wa mkoani Rukwa kwa kuzingatia makundi yao ili kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali.


 Kauli hiyo ameitoa leo mkoani hapo wakati Maafisa wa TRA walipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kumpatia taarifa kuhusu kuanza kwa kampeni ya utoaji wa elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango. Mhe Mkirikiti amesema kwamba TRA itapokua inafanya kampeni yake ya kuwatembelea wafanyabiashara katika maduka yao wahakikishe kwamba wanawapa elimu walipakodi kuhusu umuhimu wa wao kulipa kodi na kusikiliza changamoto zao mbalimbali za kibiashara.

 “Mkienda kufanya tathmini kwa walipakodi hakikisheni mnawaelimisha walipakodi kwanini anapaswa kuvuka kwasababu baadhi yao hawana elimu ya kodi na wengi wao wanaficha taarifa kwasababu biashara wanazofanya mtu hajui hata biashara yake, anajua tu biashara yake kwenye kodi na masuala mengine”, alisema Mkirikiti. 

Ameongeza kuwa, angependa kuona TRA inakusanya kodi kutoka vyanzo mbalimbali na kutoka katika makundi mbalimbali ambapo amefafanua kua katika mkoa wake, kuna vyanzo mbalimbali vya kodi na pia ni mkoa wa pili katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa pato la Taifa ukiongozwa na mkoa Mbeya. 

“Mkoa hauwezi kua na pato kubwa la Taifa wakati walipakodi wake ni wachache, hivyo kuna mahusiano makubwa katika kazi mnazofanya TRA na hali halisi ya mchango wa mkoa katika pato la Taifa”, alisema Mkirikiti. 

Kwa upande wake, Meneja wa TRA mkoani Rukwa, Bw. Fredrick Kanyilili ameeleza kuwa, kampeni hiyo inalenga kuwatembelea walipakodi katika maduka yao ili kuwatambua walipakodi ambao tayari wameshasajiliwa na kuwaelimisha kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi ili walipe kodi zao kwa hiari.

 Aidha, Mkuu wa msafara kutoka TRA Makao Makuu, Bw. Mackdonald Mwakasendile amefafanua kuwa, ziara hiyo inalenga la kutoa elimu tu na sio kwenda kuwakagua ama kuwatoza kodi wafanyabiashara wa mkoa wa Rukwa. 

Kwa upande wao walipakodi mkoani hapo wameifurahia elimu ya kodi mlango kwa mlango kwani wengi wao walikua hawajui masuala mbalimbali ya kodi na wameiomba TRA kuwa na utaratibu wa kuwatembelea katika maeneo ya biashara mara kwa mara kwasababu itawarahisishia wao kupata elimu hiyo kwa wakati badala ya kufunga safari kwenda ofisi za TRA Kampeni ya elimu kwa mlipakodi ni zoezi endelevu ambalo TRA inaendesha katika mikoa mbalimbali nchini ambapo kwa sasa zoezi hilo lipo katika mikoa ya Rukwa, Ruvuma na Njombe na lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba elimu ya kodi inawafikia walipakodi wote katika maeneo yao ili kodi stahiki iweze kukusanywa ikiwemo kuwafanya walipakodi waweze kulipa kodi zao kwa hiari.Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Fredrick Kanyilili (kushoto) Maofisa wa TRA walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuanza kampeni ya akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Joseph Mkirikitiwakati utoaji elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango 25 Oktoba, 2021 mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Joseph Mkirikiti akiongea na Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuanza kampeni ya utoaji elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango 25 Oktoba, 2021 mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Joseph Mkirikiti akiwa katika picha ya pamojana Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuanza kampeni ya utoaji elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango 25 Oktoba, 2021 mkoani Rukwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad