HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 25, 2021

MAELFU WAJITOKEZA KUPIMA SARATANI KATIKA KAMPENI YA AFYA KWANZ

  IDADI kubwa ya Wananchi wa jiji la Dar es salaam wamejitokeza kupima afya zao kupitia Kampeni ya Afya Kwanza yenye kauli mbiu ya Shtukia Fasta inayoendeshwa mjumuiko wa Taasisi za kijamii mbalimbali kwa ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika dhamira ya kuondoa tatizo la Saratani Nchini Tanzania.


Hatua hiyo imekuja kufuatia maadhimisho ya mwezi wa magonjwa ya Saratani Duniani.Taasisi hizo ambazo ni Pamoja na Inspire Consultants, Associazione Ruvuma Onlus, Shujaa Cancer Foundation, Genesis Cancer and Palliative Care Foundation,

Tanzania Comprehensive Cancer Project, Ocean Road Cancer Institute na kituo cha matangazo Clouds Media Group zimekuja Pamoja kuadhimisha mwezi huu kwa kujitoa, kuweka kambi kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma ya upimaji bure bila malipo, kwa wakazi wa maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ufunguzi wa kambi ya kwanza ya siku mbili ya upimaji bure Mbagala, mtaalam kutoka Taasisi ya Tanzania Comprehensive Cancer Project, TCCP, Dr Irene Ketegwe amesema zoezi hili linatazamiwa kupunguza gharama kubwa inayoweza

kuingiza nchi kutokana na ugunjwa huu kuchelewa kugunduliwa mapema ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya watu kupoteza Maisha.Dr. Irene Katemwa, ameeleza kuwa matibabu ya Saratani ya Matiti hutolewa kulingana na hatua za ugonjwa na hali ya mgonjwa. Amesema huduma za matibabu hutolewa kwa njia ya upasuaji katika hatua za mwanzo za

ugonjwa,mionzi,Dawa za Saratani au mionzi na dawa kwa Pamoja na ambazo gharama zake huwa mara dufu endapo mgonjwa anapochelewa kugundulika mapema.Vilevile amesisitiza kuwa wanawake wanapoona dalili zifuatazo:- kutokwa na damu baada ya kujamiana, kutokwa na uchafu sehemu za siri,kutokwa na majimaji yenye

harufu mbaya,kutokwa na usaha sehemu za siri,kutokwa na damu sehemu za siri isiyo na hedhi,maumivu ya kiuno na maumivu ya tumbo chini ya kitovu wawahi Hospitali kwani hizo ni dalili za Saratani ya Mlango wa kizazi.

Katika zoezi hilo Mtaalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road Dr Crispin Kahesa amesema‘‘Saratani ya Mlango wa kizazi ni Saratani inayoongoza kwa vifo vingi vya wanawake hapa Tanzania hivyo utaratibu wa kupima inasaidia kupunguza vifo hivyo kwani Saratani hii ikigundulika mapema inatibika’’.

Wananchi waliojitokeza kupima wameshauriwa kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo kwa kutojamiana na wanaume wengi kwani kirusi cha ugonjwa huo kinasambaa kwa njia ya kujamiana na mtu mwenye kirusi hicho, hivyo wanawake wameshauriwa kupenda na kulinda Afya zao.

Akieleza juu ya uitikiwaji wa kampeni hii ya Afya Kwanza yenye kaulimbiu ‘stukia Fasta’, Bi Happy Seiph Rwechungura mratibu wa zoezi hili alisema wananchi wengi wameamka na kuona umuhimu wa wajitokeza kupima afya zao.

Amesema “tunaowakuta na matatizo tunawapa barua ya kwenda Taasisi ya Saratani Ocean Road ili kuendelea kupata uchunguzi na tiba endelevu,”Baadhi ya wakazi wa Mbagala, Tabata, Kigamboni waliojitokeza katika kambi ya upimaji kwa ajili ya kupima viashiria vya saratani ya matiti, mlango wa kizazi na tezi dume waligundulika na viashiria waliweza kupatiwa rufaa ya kwenda kupima zaidi kwenye Taasisi ya SaratanI Ocean Road jijini Dar es salaam.

Wakazi wa maeneno mengine jijini Dar es salaam wameombwa kufuatilia zoezi hili la upimaji bila malipo katika kambi nyingine zinazoendela hapa jijini dar es salaam hadi kufikia tarehe 29 mwezi oktoba 2021. Vituo vilivyobaki ni Kimara Stop Over tarehe 25 na 26 pamoja na Tanganyika Packers, Kawe tarehe 28 na 29 Oktoba 2021.

Huduma zinazoendelea kutolewa ni pamoja na upimaji wa tezi dume, saratani ya matiti na saratani ya mlango wa kizazi.Mmoja wa wanufaika wa huduma ya upimaji wa saratani ya matiti na mlako wa
kizazi, Bi Fatuma Mikidadi amesema huduma hiyo ni nzuri na kuomba muda
uongezwe.

“Huduma ni nzuri lakini siku mbili hazitoshi kwa sababu watu ni wengi na wengine bado hawana taarifa hivyo wakisikia watakuwa wengi,” amesema Mileka

Akiongea kutoka Mbagala Zakhiem zoezi hili lilipoanzia Mmoja wa madaktari wanaotoa huduma kutoka mradi wa TCCP amesema hadi kufikia saa nne tayari walikuwa wameshawaona wagonjwa zaidi ya 300 na kwamba kutokana na wingi wa watu wanakusudia kuwahudumia hadi watu 3000 kwa muda wa siku 10.

“Tulianza shughuli saa moja lakini hadi kufikia saa 4:30 asubuhi tumeshaandikisha wagonjwa zaidi ya 300 kwa siku hizi mbili tunaweza kuwaona wagonjwa 600 kutokana na idadi ya watu kuwa kubwa, na uwezo wetu kwa eneo hili” amesema mratibu mwandamizi wa Mradi, Bi Nseya Kipilyango kutoka Taasisi ya Inspire Consultants.

Amesema katika idadi ya watu waliojitokeza wengi ni wanawake lakini hata hivyo wameshangazwa na idadi kubwa zaidi ya wanaume hasa ukichukulia kuwa kutokana na dhana potofu kuhusu upimaji mwanzaoni wanaume wengi waliogopa kujitokeza, alisema lakini baada ya uelimishaji unaondelea katika kituo cha matangazo Clouds Media Group elimu hii imesaidia kuongeza idadi hiyo yawanaume kushiriki katika zoezi la upimaji wa tezi dume ambao hufanyika kwa njiaya damu. 

“Tunashukuru serikali kwa kutupatia maeneo mazuri kwa ajili ya kutoa huduma hizi,changamoto kubwa tuliyokutana nayo ni utoaji wa huduma hii kulingana na watu wanaojitokeza, bado uhitaji ni mkubwa na uwezo wetu ni mdogo, tunaomba watu na taasisi mbalimbali kujitokeza kuchangia zoezi hili ili tuweze kufikia watu wengi zaidi.”

Waandaji wa zoezi hili wameomba msaada Pamoja na pesa taslimu wananchi na makampuni wanaweza kuchangia ili zoezi hili lifanyike Nchi nzima bila malipo.

“Tuna uhitaji mkubwa sana wa PSA Kits kwa wanaume kupima kwa njia ya damu, tents za wagonjwa kusubiri, Tunahitaji wataalamu wa Ultrasound , medical doctors na manesi kupunguza gharama za uendeshaji

Wakujitolea ili mapambano yawe endelevu kuisaidia serikali kupambana na Saratani” alisema Dr Irene Ketegwe.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad