HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 1, 2021

KMC FC KUKIPIGA TENA KESHO NA COAST UNION MKWAKWANI TANGA

 TIMU ya KMC FC, mara baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Polisi Tanzania katika Uwanja wa Black Rhino Karatu Mkoani Arusha, kesho itashuka tena katika Dimba la Mkwakwani jijini Tanga kukipiga na wagosi wa Kaya, Coast Union.


KMC FC ambao niwageni wa mchezo huo, watamenyana na kikosi hicho kuhakikisha kuwa wanazisaka alama tatu dhidi ya wapinzani hao ambao katika msimu uliopita walitoka sare katika michezo yote miwili nyumbani na ugenini.

Licha ya kuwepo kwa ushindani katika mchezo huo, lakini hadi sasa kikosi hicho cha Manispaa ya Kinondoni, kimeshafanya maandalizi ya mwisho kabisa ambapo KMC FC KUKIPIGA TENA KESHO NA COAST UNION MKWAKWANI TANGA pamoja na benchi la ufundi wamejiandaa vizuri kuhakikisha kwamba alama tatu zinapatikana katika uwanja wa Mkwakwani.

KMC FC chini ya kocha Mkuu John Simkoko pamoja na wasaidizi wake, Habibu Kondo, Hamadi Ally wameshafanya marekebisho ya makosa madogo madogo yaliyojitokeza katika mchezo uliopita na hivyo kupelekea kupoteza na kwamba katika mchezo wa kesho malengo makubwa ni kupambana ili kuhakikisha kwamba Timu inashinda.

“Tumetoka kupoteza mchezo wetu muhimu wa kwanza kabisa kwenye ligi, lakini hatujakata tamaa zaidi nikama tumepandishwa hasira, tunafahamu mchezo utakuwa mgumu, wapinzani wetu pia tunawafahamu kuwa wako vizuri, lakini haimanishi kwamba KMC tunawahofia kikubwa tunakwenda kupambana uwanjani.

“Lakini pia siku zote Timu bora huwa haipotezi mechi mara mbili, tunaamini sisi ni bora, kikosi kizima kikovizuri, hata maandalizi ambayo tumefanya jana mara baada ya kufika Jijini Tanga yalikuwa kwa ustadi mkubwa na wakuleta mafaniko ya kushinda mchezo wetu wa kesho.

Imetolewa leo Oktoba 1

Na Christina Mwagala

Afisa habari na Mawasiliano wa KMC FCa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad