HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 10, 2021

DC MKURANGA AWAASA VIJANA KUJIKITA KATIKA MICHEZO

 

Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga

MKUU wa wilaya ya Mkuranga ,Mkoani Pwani Hadija Nasir amewaasa vijana kujikita katika masuala ya michezo kwani ni sekta yenye ajira ya kujiajili kujiongezea kipato.

Alisema kwasasa soka ni ajira ambapo timu kubwa zimekuwa ushawishi mkubwa kwa kundi la vijana lililopo mashuleni na mitaa.

Hadija alitoa rai hiyo ,wakati akipokea jogging (mbio pole)octoba 9 ikiwa ni Bonanza la michezo lililoandaliwa na mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega.

Hadija aliyeambatana na kamati yake ya ulinzi na usalama wilaya ,alimpongeza Ulega kwa ratiba hiyo ya michezo.

"Kwa dunia ya sasa michezo Ni ajira,vijana mshiriki katika ajira kulinda afya na kujipatia kipato"

Mkuu huyo wa wilaya Mkuranga alieleza, mwaka juzi janga la Corona ilipoingia nchini marehemu Rais wa awamu ya tano John Magufuli alihamasisha mazoezi , nashukuru wengi wetu tuliitikia wito huu,kwahiyo mazoezi ni afya na kupunguza magonjwa "

Bonanza hilo limeambatana na zoexi la uchangiaji damu na kuchanja chanjo ya Uviko19 alihimiza kuchoma chanjo hiyo kwa hiari ili kujilinda na ugonjwa huu.

Alieleza tayari dozi nyingine zimepokelewa nchini ,na kwa Mkuranga awamu ya Kwanza dozi 4,000 iliyotolewa zimeisha.

Hadija alieleza kwasasa wamepokea dozi nyingine kwahiyo wananchi wamuunge mkono kuchanja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Kuhusu kuchangia damu alisema ni muhimu kwasababu zinasaidia kuchangia bank ya damu na wagonjwa wenye mahitaji.

Akielezea Bonanza hilo ,katibu wa mbunge wa Jimbo la Mkuranga Omary Kisatu alisema ,zoezi la uzinduzi wa Ulega cup imesindikizwa na jogging(mbio za pole) na fainali ya mchezo wa bao katika viwanja vya godown na baadae mechi ya ufunguzi wa Ulega Cup itakuwa baina ya timu ya Mipeko na Tengelea Yatakayofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkuranga.

Alisema mazoezi yanapaswa kufanywa kila siku ili kujenga afya nzuri na kupunguza magonjwa.

"Michezo pia ni ajira ,vijana changamkieni fursa hii ili kuinua vipaji na kupata ajira katika timu mbalimbali."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad