HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 10, 2021

DKT MPANGO AIKABIDHI POSTA MAGARI 18, PIKIPIKI 20, AHITIMISHA MAADHIMISHO WIKI YA POSTA DUNIANI

Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa TPC kwa ajili ya kuboresha huduma ya shirika hilo. 

Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 18 na pikipiki 20 kwa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa ajili ya kuboresha huduma za shirika hilo. Tukio hilo lilifanyika wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya Wiki ya Posta Duniani lililofanyika kitaifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH) Dkt. Ashatu Kijaji na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula.
Dkt. Mpango akiwasha moja ya magari yaliyonunuliwa na Serikali na kuikabidhi TPC.

Dkt Mpango akishuka kutoka kwenye gari hilo.
Makamu wa Rais, Dkt Mpango akimkabiudhi tuzo Mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Msalato, Renalda Reginald kwa kuwa mshindi wa kuandika insha kuhusu matumizi ya huduma mpya ya kidigitali.
Dkt. Mpango akimkabidhi tuzo mwanafunzi Faraja Robert (asiyeona) wa shule ya Buhangija ya Shinyanga baada ya kuwa mshindi wa tuzo maalumu kwa wanafunzi walioandika insha nzuri.
Dkt Mpango akimkabidhi tuzo ya cheti mwakilishi wa Benki ya CRDB wadhamini wakuu wa maadhimisho hayo.
Sehemu ya waalikwa.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamis Munkunda (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Gift Msuya.
Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika maadhimisho hayo.

Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo akielezea mikakati mbalimbali waliyofanya kuboresha huduma za shirika hilo ikiwemo uanzishwaji wa Duka la Posta Mtandaoni ambapo limeungana na maduka 670 duniani ambapo wateja wanunua na kuuza bidhaa zao mtandaoni.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Sifundo Moyo akitoa salamu za umoja huo wakati wa maadhimisho hayo.
Msanii Mrisho Mpoto ambaye ni Balozi wa Posta akitumbuiza wakati wa maadhimisho hayo.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Kijaji akizungumza maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Dkt. Mpango kuhutubia na kuhitimisha maadhimisho hayo.

Makamu wa Rais, Dkt. Mapango akihutubia wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Posta Duniani.
Dkt Mapango akiagana na viongozi mbalimbali baada kuhitimisha maadhimisho hayo.
Kikundi cha ngoma za asili cha Nyati kikitumbuiza mbele ya Makamu wa Rais, Dkt Mapango.
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akijadiliana jambo na Waziri Dkt Kijaji na Katibu Mkuu, Dkt Chaula.
Baadhi ya magari yaliyokabidhiwa kwa TPC

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad