Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede, Afisa Mtendaji
Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa
NMB, Benedicto Baragomwa, wakipata maelezo ya suluhishi mbali mbali za
mifumo ya kifedha ya Tehama kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni
changa ya tehama katika uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa
NMB. 

Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kati kati) na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna wakipata maelezo ya
suluhishi mbali mbali za mifumo ya kifedha ya Tehama kutoka kwa mmoja wa
wakilishi wa kampuni changa ya tehama, katika uzinduzi wa mfumo wa
majaribio ya kidigitali wa NMB.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede(kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Kaimu Afisa Mkuu Teknolojia na Mabadiliko ya Kidigitali wa NMB, Kwame Makundi wakipata maelezo ya suluhishi mbali mbali za mifumo ya kifedha ya tehama kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni changa ya tehama, katika uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse akizungumzza wakati
alipozindua mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kati kati) na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna wakizungumza mara
baada ya uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse akiteta jambo na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna kulia na Mkuu wa
kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB – Vicky Bishubo mara baada ya
uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

Mhazini
wa Benki ya NMB, Aziz Chacha(kushoto) na Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu
wa NMB Emmanuel Akonaay, ni miongoni ya waliohudhuria uzinduzi wa mfumo
wa majaribio ya kidigitali wa NMB uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani
City – Dar es Salaam.
***************************
Benki
ya NMB imezindua Mfumo wa Majaribio ya Suluhishi za Kidijitali (Sandbox
Environment), ikiutengea Sh. Bilioni 1 za kusaidia bunifu zitakazopita,
Mfumo ambao umepongezwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
Dk. Bernard Kibesse, na kutaka Taasisi za Fedha nchini kuiiga NMB
katika kuleta njia mbadala za kutoa suluhu za kibenki ambazo ni rahisi,
haraka na salama.
NMB
Sandbox ni jukwaa huru la NMB linalotoa fursa kwa wabunifu wa
Kidogitali na wabunifu binafsi wa Kitanzania kutumia Mifumo ya benki ya
NMB kujaribu suluhishi zao kabla ya kuanza kutumika rasmi.
Uzinduzi
huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam, ambapo Mgeni rasmi Dk. Kibesse
alisisitiza kuwa mabenki nchini hayana budi kuendana na kasi ya
mabadiliko ya tekinolojia ili kutoa suluhishi za huduma za kibenki, hasa
katika nyakati hizi, ambazo tekinolojia imetanua wigo wa kuhudumia.
“Uzinduzi
huu wa Sandbox Environment, unafungua fursa kwa Kampuni changa na
wabunifu binafsi kuonyesha ujuzi wao na kubuni suluhishi zitakazopunguza
gharama za kibenki kwa watu wote, sambamba na kutengeneza ajira kwa
vijana wa Kitanzania.
“BoT
inatambua changamoto zinazo wakabili wateja wanapotumia huduma za
kibenki, zikiwemo upatikanaji hafifu wa huduma hizo, ufinyu wa njia za
kufikisha, gharama na uelewa mdogo walionao katika masuala ya fedha.
“Serikali
kupitia BoT imechukua hatua mbalimbali kumaliza changamoto hizo na
uzinduzi huu unaashiria kuwa NMB inaunga mkono jitihada hizo, Kama
ilivyofanya kutenga Sh. Bilioni 100 za mikopo nafuu kwa wakulima,
wafugaji na wavuvi,” alisema Dk. Kibesse, akiahidi kuwa BoT itaendelea
kushirikiana na NMB katika kuboresha sera zinazotoa mwongozo na
kurahisisha ufanyaji wa biashara kwenye sekta ya kibenki.
Awali,
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema benki yake
imejidhatiti na kujipambanua kuendana na kasi ya tekinolojia kwa kuleta
suluhishi mpya zinazorahisisha huduma za kibenki kwa mteja mmoja mmoja
na wafanya biashara wadogo na wa kati, na kwamba benki yake imetenga
kiasi cha Sh. Bilioni 1 kwa ajili ya kuziwezesha suluhishi zitakazopita
katika majaribio hayo.
Zaipuna
alimhakikishia Dk. Kibese kuwa, licha ya kwamba utatumika kwa
majaribio, lakini Sanbox Environment hautoathiri kwa namna yoyote
usalama wa taarifa, amana na faragha za wateja wao na kwamba baadhi ya
tuzo za miaka ya karibuni ilizopata benki hiyo zimetokana na uwekezaji
mkubwa waliofanya katika mifumo ya Kidijitali.
“Hivi
karibuni tumeshinda Tuzo ya Benki Bora ya Ubunifu ya wateja binafsi
kutoka Jarida la Kimataifa la International Banker, huku tukiendelea
kuongoza sokoni katika kutoa huduma za kibenki kidijitali na kuongeza
bunifu Kama hizi za kuwaleta karibu wateja wetu kupitia mifumo ya
kiteknolojia.
“Tunaahidi
kuendelea kuongeza juhudi za kuhakikisha tunafikisha na kuchagiza
matumizi ya huduma za kifedha miongoni mwa Watanzania bila kujali
walipo, yote yakiwezeshwa na bunifu hizi za Kidijitali,” alisema Zaipuna
na kubainisha kuwa Sandbox Environment ni jukwaa muafaka kwa Kampuni za
Ubunifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kufanya
majaribio ya bunifu zao.
No comments:
Post a Comment