HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 22, 2021

DIT YASHUKULIWA KWA KUHAMASISHA WASICHANA KUSOMA SAYANSI NJOMBE

 Na Mwandishiwetu 

Ofisa Elimu Taaluma Sekondari wa Halmashauri ya mji wa Njombe, Huruma Chaula ameushukuru uongozi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa jitihada zake za kuhamasisha wasichana kupendelea zaidi masomo ya Sayansi ili kuongeza udahili wa watoto wa kike katika Taasisi za  elimu ya juu.


Chaula ameishukuru DIT kwa kutembelea Halmashauri ya mji huo hasa shule ya sekondari Anna Makinda kwa kuwa katika mji huo sekondari ziko nyingi,lakini Shule yao imepata fursa ya kutembelewa kwao ni siku muhimu zaidi kwa maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, na kuwataka wanafunzi wa wautumie ujumbe wa DIT kama ufunguo wa maisha yao.


"Shukrani zetu zifike pia kwa aliyeruhusu tukio hili la uhamasishaji, mabinti kusoma masomo ya Sayansi. Tumepokea neema hii kutembelewa ni nafasi ya pekee kabisa kwa wana Njombe,"alisema Chaula.


Naye Ofisa Elimu Kata ya Ihanga, Heri Mwinuka aliwaeleza wanafunzi wa kike wa Njombe kwamba wamepata bahati ya kupewa miongozo itakayowasaidia kwenda mbele zaidi.


"Nawashukuru DIT kwa ujumbe huu, tunachukulia kama chachu hasa ikizingatiwa Kata yetu ina shule tatu za sekondari, hii imepata bahati ya pekee, tunaahidi kufikisha ujumbe huu kwa shule nyingine ambazo ni Liowola na St.Joseph.

Mwinuka alisema mwaka ujao watafanya tathmini ya vijana wao wangapi waliojiunga DIT." 


Malengo ya DIT ya kuhamasisha wanafunzi wa kike wa mikoa sita (6) hapa nchini ni kufikia agenda ya nchi juu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Ofisa Elimu Taaluma Sekondari wa Halmashauri ya mji wa Njombe, Huruma Chaula, Akitoa neno la shukrani


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad