Tanzania kufaidika na mpango uliozinduliwa wa mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya kilimo-chakula Afrika - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 10, 2021

Tanzania kufaidika na mpango uliozinduliwa wa mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya kilimo-chakula Afrika

 

Mpango utakaoleta zana za kidijitali na vyanzo vya mafunzo ya kilimo kwa wakulima wadogo na biashara ndogo zinazojihusisha na kilimo barani Afrika umezinduliwa. Mpango huo umeanzishwa kwa ushirikiano baina ya Mpango wa Microsoft 4Afrika na IFC unaolenga kupiga jeki mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya kilimo-biashara barani Afrika, kuboresha mnyororo wa usambazaji na kukuza uzalishaji na pato la wakulima.

Kwa kuanzia, mfumo utakaotumia simu za mkononi utaanza kutumiwa na wakulima nchini Tanzania, Kenya, Nigeria, Cote d’Ivoire, na Uganda. Mpango huo umelenga kuwafikia na kusaidia wakulima 50,000 na vyama vya ushirika si chini ya 50. Mpango unakuja kutokana na ukweli kuwa teknolojia ya kidijitali uboresha uendeshaji wa mifumo ya minyororo ya uzambazaji katika mfumo wa chakula kupitia ufanisi mkubwa wa kilimo, uboreshwaji wa ufanyaji biashara, upatikanaji, huifadhi wa chakula na, upatikanaji wa fedha. Hata hivyo, matumizi ya zana hizi za kidijitali katika sekta ya kilimo barani Afrika bado ni madogo, kutokana na miundombinu, uwezo, uelewa, na mausala ya udhibiti. Kilimo kinachangia kiasi cha asilimia 25 ya pato la Afrika na uchangia asimilia 70 ya ajira zote.

“Sasa zaidi ya hapo awali, tunahitaji kuwa makini zaidi kwenye jinsi gani taasisi za kiteknolojia za kilimo zinafanya mabadiliko kidijitali, wanakutana na changamoto gani katika kupata teknolojia mpya, na changamoto za kila siku wanazoweza kuzipata katika eneo la maendeleo ya ujuzi wa kidijitali. Mkakati wa Microsoft 4Afrika ni kuwekeza katika teknolojia ya kilimo ili kufungua uwezo mahiri wa Afrika, kuleta ubunifu katika teknolojia ya kilimo, kuwekeza katika kilimo kitokanacho na takwimu ambacho kinaweza kuza mavuno, uzalishaji shambani na kukuza faida – vyote vikienda pamoja na kulisha taifa,” alisema Kendi Nderitu, Meneja Mkazi wa Microsoft Kenya.

Ushirikiano huo unaongezea nguvu mifumo ya kipekee ya kidijitali ya Microsoft 4Afrika na Mradi wa Uongozi wa Kilimobiashara wa IFC ili kusaidia wakulima wadogo, vyama vyao, na “wauzaji wa mwisho” kupata taarifa na zana za kidijitali katika kukiongezea nguvu kilimo, kujenga taaluma ya biashara na kuboresha akiba ya chakula na upatikanaji wake katika mnyororo wote wa usambazaji.

Kwa upande wake, Bw. Samuel Dzotefe, kaimu Mkurugenzi wa Viwanda wa Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika, Uzalishaji, Kilimo-biashara na Huduma, alisema: “Teknolojia za kidijitali zinauwezo wa kukibadirisha kilimo kidogo barani Afrika. Kwa kuzifanya zana za kidijitali kupatikana kwa wakulima, vyama vya ushirika na wauzaji wa mwisho, Microsoft na IFC kwapamoja zitasaidia sekta ya kilimo cha biashara kutumia fursa hii iliyoletwa na uchumi wa kidijitali.”

Kiasi cha watu milioni 155 walipatwa na uhaba wa chakula kwa mwaka 2020 katika nchi 55, ongezeko la karibia watu milioni 20 kutoka mwaka 2019, kwa mujibu wa Ripoti ya Mwaka 2021 ya Janga la Chakula Duniani. Katika nchi 10 zenye idadi kubwa zaidi ya watu zinazokumbana na uhaba wa chakula, sita zilikuwa ni za Afrika.

Teknolojia ya kidijitali ni moja ya njia za kukuza uzalishaji wa kilimo na ufanisi. Ushirikiano huu utajumuisha mfumo wa kuchati wa simu wa Microsoft KuzaBot, ambao utaongeza kasi na kurahisisha utoaji wa taarifa muhimu kwa wakulima juu ya ufanyaji wa kilimo bora na biashara.

Mradi wa Uongozi wa Kilimobiashara wa IFC, ambao utakuwepo kwenye mfumo wa Microsoft wa Mafunzo ya Jamii, utasaidia wafanyabiashara wadogo, wakusanya mazao, na vyama vya wakulima kuboresha taaluma zao, uzalishaji, na uwezo wa ukopeshwaji. Kwa kipindi cha muda mrefu, ushirikiano unalenga kukuza zaidi uelewa wa sababu zinazopelekea utwaaji na utumiaji wa tatuzi za kidijitali miongoni mwa wakulima wadogo, vyama vya ushirika vya wakulima, na wadau wengine husika katika mnyororo wa usambazaji wa kilimo.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad