Benki ya NMB
imetoa Sh. 60 Milioni kwa ajili ya kudhamini Mashindano Maalumu ya
mchezo wa Gofu ya Mkuu wa Majeshi (CDF ) ambayo yanatarajia kuanza
Septemba 17 hadi 19 kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu vya Lugalo Jijini
Dar es Salaam.
Mashindano hayo hufanyika kila mwaka lengo kuu
ni kuuinua mchezo huo pamoja na kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi
ili kuja kuwa tegemezi siku zijazo.
Akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi hundi Mkuu wa kitengo cha wateja maalumu wa NMB, Getrude
Mallya, alisema wanajisikia furaha kuwa sehemu ya kufanikisha kufanyika
kwa shindano hilo ambalo anaamini mwaka huu litafana kutokana na zawadi
nono ambazo zimeandaliwa kwa washindi.
Mallya alisema kiasi
hicho cha fedha kimetumika katika kununua vifaa mbalimbali vitakavyo
tumiwa na washiriki wa shindano hilo ikiwemo fulana, kofia, bendera na
zawadi za washindi ambazo zitatolewa siku ya mwisho.
“Sisi kama
NMB tunajisikia furaha kuona shindano la mwaka huu linakwenda kufanyika
kwa ubora na mafanikio ya juu kabisa nahii inathibitisha kwamba sisi
ndio Benki ambayo inaijali jamii kwa ukaribu kutokana na kudhamini
masuala mbalimbali ikiwo ya kimichezo,” alisema Mallya
Meneja
huyo pia aliupongeza uongozi wa klabu ya Lugalo, kwa imani yao kwao na
kuendeleza mchezo wa Gofu nchini kwa juhudi kubwa wanazozifanya za
kuanzisha mashindano mbalimbali na kuwachagua wao kushirikiana nao
kuyadhamini.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo
Michael Luwango, alisema zaidi ya wachezaji 170, wanatarajia kushiriki
mashindano ya mwaka huu ikiwemo vijana wadogo wa shule (Junior) ambao
wao ndio watakao fungua mashindano hayo siku ya kwanza Septemba 17.
Alisema
tofauti na miaka mingine mwaka huu wametoa nafasi ya watu mbalimbali
kushiriki michuano hiyo wakiwemo watu binfsi na wachezaji wakulipwa
pamoja na wageni endapo watajisikia kushiriki.
Kiongozi huyo
alisema mpaka sasa mwitikio kwa watu wanaoomba kushiriki ni mkubwa
ambapo zaidi ya watu 100 wameshathibitisha ushiriki wao na maandalizi
yanakwenda vizuri ikiwemo ubora wa viwanja ambavyo vitatumika kwenye
shindano hilo.
Naye Katibu wa Chama cha Gofu Tanzania Boniface
Nyiti, alisema shindano hilo la Mkuu wa Majeshi lipo kwenye kalenda ya
TGU na limekuwa na mchango mkubwa kwa taifa kutokana na kutoa wacheaji
wengi ambao wanajenga timu ya taifa.
Nyiti aliwataka viongozi wa
klabu za mchezo huo wanaoanzisha mashindano mengine kipindi ambacho
shindano la Mkuu wa Majeshi linafanyika watawachukulia hatua ikiwemo
kuwafungia kutoshiriki mchezo huo kwa kufuata sheria kwani kufanya hivyo
nikuwanyima fursa wachezaji kuto onesha uwezo wao.
Mpaka sasa
zaidi ya klabu 10 kutoka mikoa tofauti imethibitisha kushiriki michuano
hiyo baadhi yao ni Morogoro, Zanzibar, Arusha, Moshi, Dar es Salaam
Gymkhana Klubu na Lugalo .
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum Benki ya NMB, Getrude Mallya
akimakabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh.milioni 25.5 Mwenyekiti
wa Klabu ya Golf ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo
ikiwa ni udhamini wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi
'NMB CDF Trophy 2021'. Kulia ni Meneja wa Club ya Golf ya Lugalo, Luteni
Kanali, Frank Kaluwa na Meneja Mwandamizi Wateja Maalum wa NMB,
Emmanuel Mahodanga wakishuhudia. Benki ya NMB imetoa takribani milioni
60 kwa ajili ya udhamini wa mashindano hayo kiujumla kwa mwaka huu.
Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Maalum Benki ya NMB, Getrude Mallya (katikati)
akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye hafla ya kupokea mfano
wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 25.5 kwa ajili ya udhamini
wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF Trophy
2021'. Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo, Brigedia Jenerali
Mstaafu Michael Luwongo pamoja na Meneja Mwandamizi Wateja Maalum wa
NMB, Emmanuel Mahodanga (kulia) wakishuhudia.
No comments:
Post a Comment