Na John Walter -Manyara
Kufutia tukio la moto kuteketeza ofisi ya walimu katika shule secondari ya Gichameda iliyopo wilaya ya Babati mkoani Manyara,Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani hapa limeeleza chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme katika jengo hilo.
Aidha ameongeza kuwa moto huo uliunguza ofisi ya walimu na vitabu mbalimbali ambavyo viliteketea, pamoja na ofisi ya fedha huku ya makamu mkuu wa shule ambapo hata hivyo juhudi zilifanyika kuokoa nyaraka zilizpokuwemo katika ofisi hizo.
Sambamba na tukio hilo ACP Mvungi amewataka wakuu wa taasisi za umma na binafsi Mkoani Manyara kuchukua tahadhari ya moto kwa kuweka miundombinu ya kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea. Naye mwenyekiti wa kijiji cha Gichameda Alex Joseph amesema alisikia kelele za watu wakiomba msaada ndipo akafika eneo la shule na kujionea tukio hilo la moto na kushirikiana na wananchi wengine wakaendelea kuokoa sehemu ya jengo hilo pamoja na nyaraka na kumbukumbu katika ofisi ya fedha.Mwalimu mkuu wa shule hiyo ameeleza kuwa ofisi ya walimu na ofisi ya makamu mkuu wa shule ndizo zilizo athirika na moto huo, licha ya juhudi mbalimbali za kuudhibiti kufanywa na wananchi usiku wa manane.
No comments:
Post a Comment