HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 13, 2021

EQUITY BANK (T) NA PASS TRUST WAKUBALIANA DHAMANA ZA MIKOPO YA KILIMO ILI KUONGEZA NEEMA KWA WAKULIMA NCHINI

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity (T) Robert Kiboti pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Trust Yohane Kaduma wakitia saini Mkataba wa Maridhiano (MOU) ambapo Taasisi ya PASS itatoa kiasi cha shilingi Bilioni 2.3 kama dhamana ya mikopo mbalimbali ya Kilimo ili kuongeza tija na uzalishaji.

 

Dar es Salaam, Jumatatu tarehe 13 Septemba 2021. Benki ya Equity
(T) imetia saini Mkataba wa Makubaliano ya udhamini wa mikopo ya
kilimo-Biashara na Taasisi ya PASS Trust, ili kurahisisha upatikanaji wa
mikopo ya kilimo na hatimaye na kuongeza tija na uzalishaji.


Mkataba huo wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni moja ($1mn)
ulisainiwa leo jijini Dar es Salaam na utawezesha kampuni ya PASS
kutoa udhamini kwa wakopaji wa sekta ya kilimo ndani ya Benki ya
Equity kwa kuanzia asilimia 20 mpaka 80. Maoneo yatakayo faidika na
udhamini huo ni kilimo, uvuvi, ufugaji na shughuli zote katika minyonyoro
ya thamani kwa sekta kilimo ikiwemo wajasiliamari, Taasisi ndogo za
Fedha (MFIs) na vyama vya Ushirika.


Kilimo ni sekta muhimu kwa uchumi wa Tanzania, yenye kuchangia
takribani asilimia 27% ya pato la taifa na kutoa zaidi ya 75% ya ajira
zote nchini.


Akiongea katika hafla ya utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Equity (T) Robert Kiboti alisema: "Kilimo ni mhimili wa uchumi wetu.
Katika Benki ya Equity, kilimo ni eneo linalopewa kipaumbele kikubwa.
Tumeadhimia kuongeza wigo wetu wa kukopesha kwenye kilimo na
kujiwekea lengo la mikopo ya kilimo kufika asilimia 30 ya jumla la
mkopo yetu yote. Benki ya Equity, tunafurahi kuungana na washirika
wetu wa PASS katika kuhakikisha kila mtu katika mnyororo wa thamani
ya kilimo anaweza kupata fedha na mitaji inayohitajika katika kuongeza
tija na kuwezesha uzalishaji bora. Dhamira ya Benki ya Equity ni
kuhakikisha kuwa anuwai za kilimo-SME zinapata suluhisho la kifedha
katika hatua zote za mnyororo wa thamani, kutoka kwa uzalishaji hadi
maeneo ya soko. Kwa hivyo, ni muhimu kwetu kuendelea kutoa fursa za
kifedha ambazo yataweza upatikanaji wa mikopo nafuu na kwa urahisi
zaidi na hivyo kuchangia mabadiliko chanya ya kilimo, uchumi, na
maisha ya Watanzania kwa jumla, "alibainisha.


Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust, Yohane Kaduma, alipongeza
ushirikiano ulioboreshwa kati ya PASS Trust na benki ya Equity, na
kuwahamasisha wakulima na wafanyabishara kuchangamkia fursa hiyo
adimu katika kuboresha kilimo nchini Tanzania. “Kuingia kwa benki ya
Equity kwenye dhamana hii ya mikopo ya kilimo, kunaleta sasa jumla ya
benki 14 zinazoshirikiana na PASS Trust katika kuwezesha ufikishaji wa
mikopo nafuu ya kilimo kupitia mpango wa wetu wa dhamana ya
PASS. Nichukue fursa hii kualika benki nyingi zaidi kujiunga na mfumo
huu ili watanzania wengi zaidi wanaohusika katika biashara ya kilimo, waweze kupata mkopo na kuongeza uzalishaji. Kwa kuanzia, kampuni
ya PASS Trust tumetoa takriban dola milioni moja (shilingi 2.3bn) kwa
Benki ya Equity ili kufanikisha mpango huu mpya.” Alisema Bwana
Kaduma.


Katika makubaliano haya ya uendeshaji na benki ya Equity, PASS itatoa
dhamana kati ya 20-60% ya mkopo (80% kwa wanawake) kwa Benki ya
Equity ili kuongeza dhamana na kuwezesha upatikanaji mikopo kwa
urahisi. Pia Miradi ya kilimo inayoongozwa na wanawake itafaidika na
hadi dhamana ya 80% ya mkopo wa PASS. Mpaka sasa, zaidi ya
wafanyabiashara milioni 1.7 wa biashara ya kilimo wameshafaidika na
mpango wa dhamana ya mkopo wa PASS tangu ilipoanza mnamo
mwaka 2000. Tangu mwaka 2017, PASS imeshasaidia upatikanaji wa
mikopo ya kilimo inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 6.7 kwa dhamana za
Shilingi 2.6 bilioni chini ya mfumo huu wa dhamana mikopo ya mnyororo
wa kilimo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad