WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZINDUA ZOEZI LA UTOAJI CHANJO KWA WANANCHI KATIKA TAMASHA LA KIZIMKAZI KUSINI UNGUJA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 27, 2021

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZINDUA ZOEZI LA UTOAJI CHANJO KWA WANANCHI KATIKA TAMASHA LA KIZIMKAZI KUSINI UNGUJA

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui akipata chanjo ya UVIKO 19 (COVID19) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo kwa wakazi wa Mkoa wa Kusini Unguja, lililoanza leo katika viwanja vya Kizimkazi Dimbani (mji mpya), Kusini Unguja Zanzibar. Zoezi hilo linaenda sambamba na tamasha la Kizimkazi 2021 lililodhaminiwa na Benki ya CRDB.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid akipata chanjo ya UVIKO 19 (COVID19) wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo kwa wakazi wa Mkoa wa Kusini Unguja, lililoanza leo katika viwanja vya Kizimkazi Dimbani mji mpya, Kusini Unguja Zanzibar. Zoezi hilo linaenda sambamba na tamasha la Kizimkazi 2021 lililodhaminiwa na Benki ya CRDB.
Sehemu ya wananchi wa mji wa Kizimkazi na maeneo ya jirani waliojitokeza kwa lengo la kupata chanjo ya ya UVIKO 19 (COVID19), zoezi linaloendelea hivi sasa katika viwanja vya Kizimkazi Dimbani mji mpya, Kusini Unguja Zanzibar.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, wakati akitoka kupata chanjo ya UVIKO 19 (COVID19) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo kwa wakazi wa Mkoa wa Kusini Unguja, lililoanza leo katika viwanja vya Kizimkazi Dimbani (mji mpya), Kusini Unguja Zanzibar


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad