HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 5, 2021

Asasi ya wakulima Njombe NSHIDA yaja na mpango mzito kuwasaidia wawekezaji wa parachichi na Makademia

 


 Na Amiri Kilagalila,Njombe


Umoja wa wakulima wa zao laparachichi na kilimo hai kupitia asasi yao ya Njombe southern Highland delepment Association NSHDA  mkoa wa Njombe wamedhamiria kupanua wigo wa uzalishaji  wa zao hilo kwa kuwataka wawekezaji kufika mkoani Njombe  kuwekeza,ambapo asasi hiyo itachukua jukumu la kusimamia mashamba yao kuanzia kumiliki shamba  mpaka  uvunaji wa tunda hilo.

Programu hiyo inalenga kupokea wawekezaji mbalimbali wenye nia ya kuwekeza katika kilimo cha parachichi na Makademia ambao watakuwa chini ya usimamizi wa asasi hiyo ya NSHIDA inayowahakikishia upatikanaji wa mashamba na usimamizi hadi msimu wa mavuno lengo ni kuongeza uzalishaji maradufu zaidi ya sasa kutokana na uhitaji mkubwa waparachichi katika soko la dunia.

Aidha hatua hiyo imechukuliwa kutokana na wakulima wengi kukosa utaalamu wa kilimo licha ya kuwa na nia ya kuwekeza ambapo asasi hiyo chini ya mkurugenzi wake Frank Msigwa imelazimika kuzindua mfumo wa kusimamia mashamba ya wakulima kuanzia hatua ya awali hadi mavuno kwa gharama ndogo.

“Kutokana na uhitaji mkubwa sana wa parachichi na Makademia duniani tumeona tuanzishe hii program ili tuweze kuwasaidia watanzania wenzetu na wasio watanzania wanaopenda kuwekeza kwenye zao hili ili tuweze kujitosheleza soko kwasababu sasa hivi matunda yamekwisha na soko limefunguka,wanunuzi wanakuja na mamilioni ya pesa na kurudi nayo kwasababu matunda hakuna ila Njombe tuna ardhi ya kutosha”alisema Frank Msigwa

Baadhi ya wakulima wa parachichi mkoani  Njombe akiwemo Godfrey Nyagawa na Lusi Zabron wamepongeza kuanzishwa kwa mfumo huo wa kuwasaidia wakulima wanao  vutiwa kuwekeza katika kilimo cha parachichi  huku wakisema utasaidia kukuza uchumi wa familia na mkoa  kwa ujumla kutokana na uhitaji mkubwa wa parachichi kwa sasa.

“Program hii itasaidia sana kukuza uchumi kupitia kwenye kilimo hiki hususani kwenye familia lakini pia itaongeza uzalishaji wa zao hili kwa kufanya matunda yaongezeke kwa wingi kwasababu hayatoshelezi kwa sasa”alisema Godfrey Nyagawa

Baadhi ya Vijana Ambao  wamejiajiri kwenye kilimo cha zao la Parachichi   amewaasa vijana waache kulalamika juu ya ugumu wa maisha  bali wachangamkie fursa mbalimbali zilizopo kwenye maeneo yao ikiwemo kuwekeza kwenye kilimo hicho

“Fursa kwenye hiki kilimo zimekuwa ni kubwa niwashauri vijana wenzangu kuwekeza kwenye hiki kilimo kwasababu mtaji ni mdogo kwa kuwekeza miche michache michache na hata kama kuna changamoto basi NSHIDA wameleta huu mpango ambao unaweza ukawekeza kwa kusimamiwa nao kwasababu wao wana uzoefu wa kutosha”alisema mmoja wa kijana aliyewekeza kwenye kilimo hicho.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad