HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 5, 2021

WAZIRI MHAGAMA AITAKA PSSSF KUEPUSHA USUMBUFU USIO WA LAZIMA KWA WASTAAFU WANAODAI MAFAO YAO

 

SERIKALI imeutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma nchini PSSSF kuendelea na mipango yake mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa umma katika maeneo ya msingi kama vile uanachama na uchangiaji, ulipaji wa mafao na mambo mengine muhimu ya kuzingatia wakiwa katika ajira, wakati wa kustaafu na baada ya kustaafu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama wakati akifunga semina za wastaafu watarajiwa zilizoandaliwa na PSSSF na kufanyika Dar es Salaam.

Waziri Mhagama ameuelekeza mfuko huo kuepusha usumbufu usio na lazima kwa wazee wanaodai mafao huku pia akiwataka kuhifadhi taarifa zao vizuri na waziuishe kwa mara kwa mara ili kuepusha ucheleweshaji wa mafao mwanachama anapostaafu.

Amesema kwa upande wao kama Serikali wanaimani kwamba sekina hizo zitaleta tija kwa wastaafu wote nchini ambapo ameongeza kuwa matarajio yao ni kuona kwamba pensheni inamsaidia Mstaafu kuishi maisha bora kama ambavyo alikua mtumishi.

"Nitoe wito kwa wastaafu mnapoamua kutumia mafao yenu kuwekeza basi ni vema mfanye uwekezaji sahihi, uwekezaji makini na pia muwekeze kwenye aina ya biashara mnayoielewa vema, mfano mtu umefanya kazi muda mrefu Dodoma ni wazi ukiwekeza kwenye kilimo cha Zabibu utakua unakielewa vema," Amesema Mhagama.

Ametoa wito pia Kwa Menejimenti za Mabenki nchini kuangalia mifumo yao vema ili kupunguza wimbi la matapeli ambao wamekua wakiwapigia simu wastaafu wakiwa na taarifa zao na kisha kuwahadaa kutoa fedha.

" Naomba Menejimenti za Mifuko na Wakuu wa Mabenki yetu leo tujiulize matapeli hawa wanapatiwa taarifa na nani, je ni watumishi wetu wasiowaadilifu au watu wengine humo kwenye Ofisi zetu tuliowaamini na kuwaacha waingie popote?

Ninajiuliza uvujaji wa taarifa hizi unatoka wapi Kama tatizo linaanzia kwa waajiri au mifumo yetu ya TEHAMA ni vema tujue na kudhibiti ili kumaliza malalamiko haya," Amesema Waziri Mhagama.

Ameutaka Mfuko wa PSSSF kuendelea na semina hizo mara kwa mara kwani kwa kufanya hivyo watakua wanawatendea haki wanachama wao ambao wengi hawana elimu ya kutosha ya usimamizi wa fedha na ubunifu wa miradi.

Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu (Kazi, Ajira,bunge ,Uratibu, Vijana na wenye ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza katika ufunguzi wa Semina ya siku mbili kwa wastaafu Watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi waa Umma (PSSSF) leo jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad