HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 16, 2021

KUNDI LA WATOTO LAASWA KUJILINDA, KUJITAMBUA, KUJITHAMINI

 

 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

KUNDI la Watoto nchini limetakiwa kujilinda, kujitambua na kujithamini katika masuala mbalimbali yanayohusu malezi na makuzi yao sambamba na kutoa taarifa pale wanapofanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Hayo yameelezwa na Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Jiji la Ilala, Suzan Madesa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto Wa Afrika ambayo yamefanyika katika  Kituo Cha Taarifa na Maarifa Kitunda, Dar es Salaam kilichopo chini ya TGNP.

Madesa amewaasa Watoto hao kupinga vitendo vya unyanyasaji na kuwa na ndoto katika maisha yao, ili kufika malengo, “Pingeni na pigeni vita vitendo kama vya Ubakaji pengine mbakaji ana maambukizi ya HIV, kama ukitoa taarifa kama umefanyiwa vitendo hivyo unaweza pata matibabu na ukapona”, amesema.

Kila ifikapo June 16 ya kila mwaka, Tanzania inaungana na Mataifa mengine kimataifa kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Siku hii ambayo chimbuko lake ni kumbukumbu ya watoto zaidi 2000 waliuawa wakati wakiandamana kupinga ubaguzi wa rangi katika mfumo wa elimu nchini Afrika Kusini mnamo mwaka 1976. 

Maadhimisho hayo kwa hapa nchini Tanzania yanafanyika katika ngazi ya Halmashauri ili kuwawezesha wananchi kwa wingi wao kushiriki maadhimisho hayo.

Mwaka huu kauli mbiu ya Siku ya Mtoto wa Afrika inasema, "Tutekeleze ajenda 2040 kwa Afrika inayolinda haki za mtoto"

Afisa ustawi wa Jamii kutoka jiji la Ilala, Suzan Madesa akitoa hotuba pamoja na kutoa mafunzo kwa watoto waliofika kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kitunda Jijini Dar es Salaam leo.
Mratibu wa elemu Kata ya Kitunda  Festo Muhimila akizungumza na watoto pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto Wa Afrika ambayo yamefanyika katika  Kituo Cha Taarifa na Maarifa Kitunda, Dar es Salaam kilichopo chini ya TGNP
Mwakilishi Mkazi wa ALARM Tanzania, John Wambura akizungumza na watoto pamoja na kuuliza maswali mbalimbali yaliyokuwa yanahusu ukatili wa kijinsia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto Wa Afrika ambayo yamefanyika katika  Kituo Cha Taarifa na Maarifa Kitunda, Dar es Salaam kilichopo chini ya TGNP
Baadhi ya watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto Wa Afrika ambayo yamefanyika katika  Kituo Cha Taarifa na Maarifa Kitunda, Dar es Salaam kilichopo chini ya TGNP
Watoto mbalimbali wakiwa wamebaba mabango yanayohusu haki zao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto Wa Afrika ambayo yamefanyika katika  Kituo Cha Taarifa na Maarifa Kitunda, Dar es Salaam kilichopo chini ya TGNP  
Picha za juu na chini ni baadhi ya michezo iliyokuwa ikichezwa ikiwemo maigizo, ngojera, mpira wa miguu, rede, kukimbia pamoja na kukimbia.Yote hata yamefanyika leo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtori wa Afrika yaliyofanyika Kitunda leo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad