Ecobank Tanzania yazindua mpango maalumu wa kuwainua Wanawake - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 5, 2021

Ecobank Tanzania yazindua mpango maalumu wa kuwainua WanawakeEcobank Tanzania imezundua rasmi mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’ wenye lengo la kuwasaidia na kuwainua Wanawake Wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa katika masuala mbalimbali ya kifedha na kuwaongezea kipato ili waweze kumudu biashara zao na kuinua vipato vyao.

Mpango huo ni maalum kwa Benki hiyo kuwaelimisha Wanawake hao jinsi ya kufanya biashara hizo sambamba na kuwapa mikopo kwa bei nafuu. Ili kuwa na vigezo ni lazima Wanawake hao Wajasiriamali wawe na Leseni za Biashara na kufungua Akaunti katika Benki hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Charles Asiedu amesema mpango huo ni maalum ambao utawaidia wanawake wajasiriamali kuongeza mtaji wao, kupata faida na kujinua kiuchumi.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa amesema mpango huo ni fursa kwa Wanawake wajasiriamali hivyo ametoa wito kwa Wanawake hao kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Ecobank Tanzania.

Bi. Beng’i amesema fursa hiyo itawapa Wanawake hao maendeleo ya kijamii na Kiuchumi hivyo kupelekea idadi kubwa ya ajira kwa vizazi vijavyo katika nyanja hizo hususan katika biashara.

Malengo ya Ecobank kuwafikia wafanya biashara wanawake wanaomiliki biashara zao na waajiriwa.

Makundi / walengwa

· Biashara zinazomilikiwa na wanawake

· Biashara zinazoendeshwa na wanawake

· Kampuni zenye asilimia kubwa ya wanawake wafanyakazi ambambo kuna managerial members / position and board members

· Kampuni zinazozalisha bidhaa za wanawake kama vile urembo mavazi n.k

Bidhaa na makampuni yanayozalisha bidhaa za wanawake

Kwa maelezo Zaidi; tembelea matawi ya Ecobank yaliyopo Dar es Salaam, Mwanza na Arusha au piga simu 0800110021 au tuma email www.ecobank.com/elevate
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad