HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 12, 2021

MAKUNDI YA WAKULIMA , WAFUGAJI YA VAMIA ENEO LA USHOROBA WA MAZALIA YA WANYAMAPORI HIFADHI YA TAIFA YA NYERERE

 



Na John Nditi, Morogoro
MAMIA ya wakulima na wafugaji wamevamia hifadhi za Jamii ya Jukumu iliyotengwa kutoka kwenye vijiji 11 vya Tarafa ya Bwakila, halmashauri ya wilaya ya Morogoro ambavyo vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na kuendesha shughuli za kilimo cha mashamba makubwa, ufugaji na makazi ya watu na kuadhiri maeneo maalumu ya ushoroba wa mazalia ya wanyamapori.

Uvamizi huo wamebinika baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Morogoro kwa kushirikiana na Maofisa wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere chini ya mkuu wa wilaya hiyo Bakari Msulwa, kufanya doria na ukaguzi wa eneo la hifadhi hizo kwa kutumia Ndege na kubainika kuwepo kwa uvamizi huo .

Baada ya ukaguzi huo Mkuu wa wilaya alitoa tamko ya serikali ya wilaya na kusema kuanzia sasa watasimamia sheria iliyopo na wananchi waliopo katika hayo maeneo na hasa yanayopakana na hifadhi hakuna njia nyingine isipo kuwa ni kuondoka na wasipofanya hivyo sheria zipo wazi za kuwaondoa.

“ Sasa wito wetu ni mmoja kwa sababu kimsingi hatufanyi jambo jipya zipo sheria zilizounda hifadhi za Taifa , sheria ambazo zinazozimamia madeneo maalumu yanayotakiwa kuhifadhiwa na hizo sheria lazima zizimamiwe” alisema Msulwa.

Mkuu wa wilaya ,alisema; “ Tukiharibu huu ushoroba ambao kwa kweli ni mazalia ya wanyamapori na vyanzo vya mito ambayo si t u inasaidia hifadhi hii kiikolojia kuendela lakini pia maji haya yanatumika kwa maeneo mengine na tusipofanya hivyo ni kosa” alisema Msulwa.

Hata hivyo , alisema Jumuiya hiyo maalumu iliundwa kisheria ambayo inaunganishwa na vijiji 11 na jukumu lake la msingi ni kuulinda huo ushoroba ambapo na kimsingi unatumiwa na wanyamapori , kiuhifadhi maji na viumbe hai vilivyopo , lakini bahati mbaya sehemu kubwa la eneo hilo la hifadhi limeharibiwa na shughuli za kibinadamu.

Mkuu wa wilaya hiyo, alisema katika ukaguzi wa doria hiyo imebainia piia eneo la hifadhi ya Jamii imejaa mifugo mingi licha ya kuwepo kwa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji hivyo .

Msulwa , alisema kwa sasa ni wajibu wa vijiji hivyo kuhakikisha vinatenga maeneo ya makazi , kilimo na mifugo ili kusiwepo kwa mifugo ndani ya hifadhi ya jamii na hifadhi ya Taifa ya Nyerere kwani hifadhi hizo zina umihimu mkubwa kwa ajili ya utalii na unaleta fedha za kigeni na utuzaji wa ikokojia .

Mkuu wa wilaya ,alisema kwa sasa wataanza kampeni maalumu ya kutoa elimu kwa wananchi kwa kufanya mikutano ya hadhara ya kuelimisha juu ya umuhimu wa kutunza rasilimali za taifa na pia kutumiza wajibu wao na pale patakapohitajika kutumia sheria ya kuwaondoa watu itatumika, lakini uwepo wa kushirikiana wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere , Mikumi , Jumuiya za wananchi na viongozi kazi hiyo itafanyika vizuri.

Naye Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, Stephano Msumi , akilezea athari zinazotokana na uvamizi katika hifadhi hizo ni uvunaji haramu wa rasilimali za Taifa kinyume na sheria za nchi.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, alitolea mfano kuwa katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2020 jumla ya majangili 112 walikamatwa ,ng’ombe 4,425 na kati ya hizo 2,950 ni kutoka wafugaji wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro na vitu vingine zikiwemo pikipiki .

Hivyo alitaja mikakati ya kukabiliana na ujangili kwenye hifadhi hiyo ni pamoja na kuhakikisha Intelejensia inatumika katika kuongoza doria zao kwa kushirikiana na wadau wengine .

Msumi, alitaja eneo ligine ni kuongeza juhudi za kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii ikiwa na pamoja na kuendelea kushirikiana na wananchi waishio maeneo yanayopakana na hifadhi hiyo.

Kwa upande wake Ofisa Maliasili na Utalii wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro , Wahida Beleko , halmashauri hiyo imenza kuchukua hatua za kuhakikisha hifadhi hiyo yenye ukubwa wa kilometa za mraba 643 inalidwa na linakuwa salama kwa kushirikisha viongozi wa vijiji 11 na wavamizi wanaondoka maeneo ya hifadhi.

Beleko ,alitaja vijiji vilivyotoa eneo la ardhi na vinavyounda Jumuiya ya Jukumu (WMA) kwa mujibu wa sheria ni kijiji cha Bonye, Mbwade, Dakawa, Bwila Chini , Bwila Juu, Magogoni, Kongwa, Kisaki Gomero, Nyarutanga , Kiburumo na Kidunda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad