Kiduku kuzipiga na Tshibangu Kayembe Machi 19 Ubungo Plaza - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 12 March 2021

Kiduku kuzipiga na Tshibangu Kayembe Machi 19 Ubungo Plaza

 

Na Mwandishi wetu
BONDIA nyota nchini, Twaha Kiduku atapambana na Tshibangu Kayembe wa DR Congo katika pambano la kimataifa la uzito wa Super Welter lililopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza Machi 19.

Pambano hilo limendaliwa na promota Evarist Ernest wa kampuni ya Mopao Entertainment na kabla ya hapo,bondia Jones Segu atatetea mkanda wake wa WBF wa uzito wa Light dhidi ya bondia kutoka Malawi Hanock Phiri.

Akizungumza jijini jana, Ernest alisema kuwa maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na mabondia wan je ya nchi watawasili nchini Machi 15 tayari kwa pambano hilo.

Alisema kuwa wanatarajia kuwa na mapambano makali na kusisimua kutokana na ubora wa mabondia wote.

“Tshibangu Kayembe alipambana na Hassan Mwakinyo kuwania mkanda wa WBF kwenye ukumbi wa Mlimani City na kupigwa kwa pointi. Bondia huyo wa DR Congo anakuja kulipiza kisasi kwa Kiduku ambaye anataka kurejesha hadhi yake baada ya kupoteza pambano nchini Misri hivi karibuni,” alisema Evarist.

Kwa upande wake, Kiduku alitamba kuwa atamchapa mpinzani wake kabla ya raundi 10 kumalizika.

“Nimejiandaa vyema na lengo langu ni kushinda kwa knockout (KO), Kayembe ni bondia mzuri sana, anajua kuzipanga ngumi zake, nitakuwa makini wakati wote,” alisema Kiduku.

Kwa upande wake Segu, alisema kuwa amejiandaa vyema kutetea mkanda wake ambao aliutwaa nchini Afrika Kusini.

“Nimeutwaa mkanda huu nje ya nchi, kamwe sitaweza kuupoteza hapa nyumbani. Phiri atarejea nchini kwake Malawi kama alivyokuja,” alisema Segu.

Mbali ya pambano hilo, siku hiyo pia akina dada Halima Bandola na Najma Isike watapanda ulingoni katika pambano la uzito wa light la raundi nne.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad