Na Woinde Shizza , Michuzi Tv-Arusha
Zaidi
ya wakulima 8000 wamenufaika na mikopo ya kilimo kutoka katika mradi wa
mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo wadogo inayodhaminiwa na benki ya
maendeleo ya kilimo (TADB) kwa kushirikiana na taasisi nyingine za
kifedha 10.
Akiongea na
waandishi wa habari Katika maonesho ya nne ya mifuko ya programu za
uwezeshaji yanayoendelea mkoani Arusha Afisa mwandamizi wa benki ya
maendeleo ya kilimo George Nyamrunda, alisema kuwa mfuko huo ni mfuko
unaoratibiwa na benki hiyo kwa ajili ya kuhamasisha au kuchagiza benki na
taasisi nyingine za fedha ziweze kukopesha wakulima.
Alisema
kuwa kwa muda mrefu wakulima wamekuwa wakikosa uwezeshaji kupitia
mabenki wakiambiwa kuwa hawakopesheki kwa sababu hawana dhamana hivyo
benki hiyo kupitia mfuko huo wamekuwaja na suluhu ya kuwapatia dhamana
mabenki Ili waweze kukopesha wakulima.
“Mpaka
sasa tuna ushirika na tasisi za kifedha kumi ambazo tunawapatia dhamana
na wao waweze kuongeza uwekezaji katika kilimo ambapo kinachofanyika ni
mabenki yanakopesha wakulima alafu benki ya kilimo inatoa dhamana na
wakishindwa kulipa tunafidia ile hasara ambayo mabenki yamepata,”
Alisema Nyamrunda.
Alieleza
wameshadhamini mikopo ya zaidi bilioni 69 kwa muda wa miaka miwili
tangu kuanzishwa kea mfuko huo ambapo wameweza kuwafikia wanufaika 8500
huku asilimia 95 wakiwa ni wakulima wadogo.
Alifafanua
kuwa lengo la mfuko huo ni kuhamasisha mabenki mengine kuisaidia benki
ya kilimo ambayo ndio inajukumu la kuwezesha sekta ya kilimo lakini
kutokana na uhitaji wa mitaji kikubwa wakahamasisha na mabenki mengine
kuwekeza.
Aliendelea
kusema kuwa faida kubwa waliyopata mpaka sasa ni kushusha ribya ya
mikopo inayotolewa kwa wakulima kutoka Asilimia 20 hadi 24 na kufikia
Asilimia 14 hadi 17.
Kwa
upande wake Lucius Mtewele meneja mikopo ya kilimo kutoka benki ya TPB
alisema kuwa wanategemea mashirikiano hayo Katika kuendeleza kilimo na
wanaamini wataweza kuwafikia wakulima wengi zaidi na kunyanyua maisha
yao.
Naye meneja
mahusiano kilimo biashara kutoka benki ya CRDB kanda ya kaskazini
Rogers Mselle ushirikiano huo umeweza kuwasaidia kuwafulikia wakulima
wengi zaidi na kuweza kuwafikia wakulima na kutoa mkopo zaidi ya bilioni
15 kupitia dhama iliyotolewa na benki ya maendeleo ya kilimo na
kufikia wanufaika 1200.
Afisa
mwandamizi wa benki ya maendeleo ya kilimo George Nyamrunda akiongea na
waandishi wa habari katika maonesho ya nne ya mifuko ya programu za
uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika Katika viwanja vya kumbukumbu
ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
Meneja mikopo ya kilimo kutoka benki ya TPB,Lucius Mtewele akiongea na waandishi wa habari katika maonesho hayo.meneja mahusiano
kilimo biashara kutoka benki ya CRDB kanda ya kaskazini Rogers Mselle
akiongea na waandishi wa habari Katika maonesho ya nne ya mifuko ya
uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika Katika viwanja vya Sheikh
Amri Abeid mkoani Arusha.
No comments:
Post a Comment