Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa Mbopo kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni,
Mohamed Bushir akizungumza na wazazi, walezi leo tarehe 9 Februari
2021. katika mkutano wa kujadili masuala mbalimbali kuhusina na
maendeleo ya shule, mkutano ulifanyika katika viwanja vya shule ya
Sekondari ya Mbopo.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa Mbopo kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni,
Mohamed Bushir akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.
Mwalim
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbopo,Jackson Mlinda akisoma hotuba yake
katika mkutano huu uliofanyi tarehe 9 Februari 2021 kwenye viwanja vya
shule hiiyo
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Na Mwandishi wetu, Michuzi TV
WANANCHI
wa Mtaa wa Mbopo uliopo Kata ya Mabwepande wilayani Kinondoni jijini
Dar es Salaam wamekutana kwenye kikao cha kuweka mikakati na mipango ya
shuleta na maedeleo katika mtaa wao huku wakitumia nafasi hiyo
kumpongeza Mbunge wao kutoka Jimbo la Kawe,Askofu Josephat Gwajima kwa
kutimiza ahadi yake kwa kuwapatia gari.
Wakizungumza
leo wakati wa kikao hicho ambacho kimefanyika katika Shule ya Sekondari
Mbopo wametumia nafasi hiyo kuzungumzia namna ambavyo wamejipanga
katika kuhakikikisha wanapata maendeleo.
Pia
wamezungumzia mikakati ya wananchi ambavyo wanaweza kushirikiana na
uongozi wa Shule ya Sekondari Mbopo kutatua baadhi ya changamoto
zilizopo.
Akizingumza
na Michuzi TV, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbopo,Mohamed Bushir
amesema kwamba wamekutana leo kwenye kikao ambacho kimewashirikisha
wananchi kwa ajili ya kujadili mipango na mikakati ya maendeleo ya shule
yao pamoja na mtaa wao.
"Tulikuwa
nachangamoto kubwa ya usafiri ambayo ilikuwa inawakabili wananchi wetu,
hasa kutoka Mabwepande, Bunju mpaka Mbopo mpaka kuiapata Madale na
Nyuki .Lakini tayari tumefanya mawasiliano na Diwani wa Kata yetu na
ametueleza ameshafanya mawasiliano na Mbunge wetu Askofu Gwajima ambaye
ameshakabidhi gari.
"Tunamshukuru
Mbunge kwa kutatua changomoto ya usafiri, ni changamoto ya muda mrefu,
bahati nzuiri miundombinu ya barabara iko vizuri kwani iko kwa kiwango
cha changarawe na tayari Serikali imeanza mkakati wa kujenga baadhi ya
barabara zetu kwa kiwango cha lami,"amesema Bushir na kusisitiza kupitia
kikao hicho wamejadilia mambo mengi ya maendeleo ya mtaa wao.
Kwa
upande wake Mwalim Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbopo Jackson Mlinda
amesema katika kikao hicho wamezungumzia maendeleo ya shule hiyo na
kikubwa ambacho wamekiomba kutoka kwa wazazi na walezi ni ushirikiano
ili kutimiza yale ambayo wamekubaliana katika kikao hicho.
"Tukishirikiana
kwa umoja wetu , tutapiga hatua ya maendeleo kwa haraka zaidi, hivyo
tunawaomba wazazi tulichokubaliana basi tutimize kwa pamoja,"amesema.
Wakati
huo huo mwananchi Philip Mushi ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano
chini ya Rais John Magufuli kwa kutoa elimu bure kuanzia elimu ya msingi
hadi sekondari kwani kwa kufanya hivyo imewapunguzia mzigo wananchi.
Aidha
Mwamvita Juma ambaye ni miongoni mwa wananchi wa mtaa huo ametoa ombi
kwa Serikali kuhakikisha mabweni ya wanafunzi katika shule ya Sekondari
Mbopo yanakamilika kwani hivi sasa wanalipa Sh.milioni 1.2 kwa mwaka
kulipia gharama za hosteli.
"Tunaomba
Serikali isimamie hosteli ya shule iishe ili wanafunzi waweze kukaa
shuleni ili kuondoka na gharama kubwa ambayo wazazi tunalipa, kila mwezi
tunalipa Sh.100,000,"amefafanua.
Kwa
upande wake Rehema Msola amemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa elimu
bure, kwani amewakwamua watu wa chini.Pia ametoa shukrani kwa Mbunge wa
Jimbo la KaweAskofu Josephat Gwajima kwa kuwapelekea usafiri kwani kwa
muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya usafiri.
No comments:
Post a Comment