NAIBU
Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amekutana na kufanya
mazungumzo na wadau wa sekta nguo na mavazi ili kusikiliza changamoto
wanazokutana nazo na mapendekezo yao katika kuboresha na kukuza sekta
hiyo.
Akizungumza na wadau hao katika kikao
kilichofanyika Februari 9, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE
) jijini Dodoma Naibu Waziri amewaagiza kuwasilisha changamoto
walizonazo na rasimu za mipango mikakati ya kuboresha na kuendeleza
Viwanda na Biashara katika sekta hiyo ili kukuza uchumi wa nchi.
Katika
kikao hicho kilichojumuisha wadau ambao ni watengenezaji na waagizaji
wa nguo na mavazi kutoka nje ya nchi, wadau hao waliwasilisha changamoto
na mapendekezo yao kwa Naibu Waziri wakiwa na lengo la kuboresha na
kukuza sekta hiyo.
Amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada
mbalimbali katika kuendeleza sekta ya nguo na mavazi nchini ikiwemo
kukuza soko la ndani la bidhaa hizo pamoja na kuandaa na kutekeleza
mkakati wa kuendeleza Sekta ya pamba nguo hadi mavazi ( Cotton to
Clothing Strategy C2C 2016 - 2020 ) na kuuhuisha ambapo utekelezaji wake
utaanza mwaka 2021 - 2032.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akiongea na wadau wa Sekta ya Nguo na Mavazi alipokutana nao ili ksikiliza changamoto wanazokutana nazo katika uendelezaji wa Viwanda na biashara ya nguo na mavazi nchini kwenye kikao kazi cha pamoja Februari 9, 2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya waagizaji wa nguo na mavazi hususani vitenge kutoka nje ya nchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika 9 Februari 9, 2021 jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment