HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 10, 2021

WILAYA YA MUFINDI YAWAPONGEZA SAO HILL KWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

 

Afisa tawala ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi,Joseph Mchina akiongea mbele ya wananchi wakati wa kugawa miti iliyotolewa na Sao Hill




Na Fredy Mgunda,Iringa.


UONGOZI wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umeupongeza wa uongozi shamba la miti la Sao Hill kwa kuendelea kutunza mazingira kwa kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo hata nje ya wilaya hiyo.

Akizungumza kwa niaba mkuu wa wilaya ya Mufindi,afisa tawala ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi,Joseph Mchina alisema kuwa kukiwa na miti utapata faida nyingi kama vile ukiwa na miti utapata hewa safi,ajira,mvua,chakula,matunda,moto rutuba kwenye udogo na ukiwa na miti utapata mazingira mazuri ya kuishi.

Alisema kuwa unapoukuta mti sehemu yeyote ile unatakiwa kuutunza na kuuthamini kutokana na thamani yake katika maisha ya mwanadamu hutengemea miti kwa namna yeyote ile na amewapongeza wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kupitia shamba la miti la Sao Hill.

Mchina aliwaomba wananchi kuacha tabia ya kukata miti ya asili hovyo ili kuepuka kuharibu mazingira kwa makusudi na kuleta madhara makubwa katika maisha ya binadamu hivyo inakiwa kila mwananchi kuendelea kutoa elimu kwa kila mtu ambaye hana elimu ya umuhimu wa miti.

“Ninaamini kuwa hakuna mtu ambaye hajui umuhimu wa misitu kwa kuwa hakuna kiumbe chochote kile duniani ambacho hakitui misitu au miti katika kuendesha maisha yake hivyo ni mhimu kila mtu kuhakikisha anatunza miti na mazingira” alisema Mchina

Aidha Mchina alisema kuwa kitendo cha viongozi wa shamba la Sao Hill kutoa miche ya miti milioni moja bure kwa wananchi wa wilaya hiyo ni kukuza uchumi kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi na Tanzania kwa ujumla kutokana na faida za miti.

Alisema kuwa uwepo wa shamba la miti katika shamba hilo la serikali limechangia kwa kiasi kikubwa kuwashawishi wananchi wengine wa wilaya hiyo kuanza kupanda miti na hadi hii leo bado wanapanda miti na umekuwa uchumi wa wananchi.

Mchina alisema kuwa kitendo cha kutoa miti hilo bure kunawakumbusha wananchi kuendelea kupanda miti kwenye mashamba yao ili kuendeleza utamaduni wa kupanda miti ili kukuza uchumi kwa wananchi wanaolizunguka samba hilo.

“Ni vema tukaendelea kutunza miti ya asili na kuendelea kupanda miti kwa kitaalamu kwa kufuata maelezo kutoka kwa wataalam ili kupunguza uharibu unaosababishwa na sisi wenyewe kwani misitu ni mali na uhai vile vile” alisema

Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuendelea kupanda miti na kuitunza ili kulinda mazingira na kukuza uchumi kwa wananchi na amewapongeza viongozi wa shamba la miti la Sao Hill kwa jitihada za kuendelea kutunza mazingira.

Nao wadau wa mazingira kutoka Shamba la Miti Sao hill wameeleza namna wanavyonukaika na uwepo wa shamba hilo la Serikali huku wakipongeza hatua zinazochukuliwa hasa juu ya ulinzi wa mazingira.

Awali Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita alisema kuwa jukumu la kila mmoja kuendelea kuyatunza mazingira na hasa juu ya ulinzi wa Bayoanuai zilizopo ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa viumbe hai wote wakiwamo Binaadam huku
akitaja za kutoweka kwa bayoanuai

Mwita alieleza namna ambavyo Shamba la Miti Sao Hill linavyohamasisha jamii kuendelea kuyatunza mazingira kwa kuihusisha katika shughuli rafiki za uhifadhi wa masitu ikiwamo ajira na ufugaji wa nyuki.

Alisema kuwa misiti imekuwa na faida mbalimbali kwa viumbe vyote duniani ikiwepo kuwa makazi ya wadudu,wanyama,ndege na eneo sahihi kujipatia chakula,ikolojia ya misitu ya Sao Hill imechangia sana upatikanaji wa maji ya mto Ruaha Mkuu na Ruaha Mdogo ambavyo hupeleka maji katika vituo vya kuzalishia umeme.

“Umeme unazalishwa katika vituo vya Mtera,Kihansi na mwalimu Nyerere wanategemea maji kutoka katoka hidhafi ya misitu ya Sao Hill kutokana na utunzaji bora wa ikolojia yake”alisema

Alisema upandaji wa miti unasaidia upatikanaji wa dawa mbalimbali za asili ambazo zimekuwa zinasaidia katika maisha ya binadam hivyo misiti inaumuhimu mkubwa sana kwa wananchi kote ulimwenguni.

Aidha Mwita alisema kuwa shamba la miti la Sao Hill limekuwa lanachangia kukuza uchumi katika sekta mbalimbali kama viwanda,miundombinu na sekta ya ujenzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad