Hayo
yamesemwa leo na Mwanasheria kutoka Kituo cha Misaada wa Sheria kwa
Wanawake na Mratibu Uwezeshaji jamii kwenye masuala ya haki na sheria
na ajira hususan kwa makundi ya vijana na wanawake, (WLAC) Consolata
Kikoti wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wafanyakazi wa sekta binafsi
na za umma ili kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao jijini Dar es
Salaam.
Amesema kumekuwa na wimbi kubwa la uelewa wa sheria na haki za wafanyakazi zinazokiukwa.
Changamoto
nyingine ni usimamizi na utekelezaji wa sheria, kutokuwepo uwajibikaji
katika kuhakikisha sheria hizo zinatekelezwa hasa katika taasisi.
Pia amesema vyama vya kutetea wafanyakazi vinatakiwa kusimamia haki hizo.
"Mafunzo
haya ya siku moja yaliyoandaliwa na kituo cha msaada wa Sheria kwa
Wanawake (WLAC) yamewashirikisha Chama cha waajiri na wadau wanaohusika
na masuala ya wafanyakazi na lengo ni kuwaweka pamoja kuona namna
watakavyowasaidia wafanyakazi na kusimamia haki za wafanyakazi katika
maeneo yao," amesema Kikoti.
Naye, Katibu wa Chama cha Walimu
Tanzania (CWT), Wilaya ya Ilala, Vicky Kibona amesema haki za
wafanyakazi zifuatwe kwani waajiri wamekuwa wakiwaachisha wafanyakazi
bila kufuata utaratibu.
Amesema sheria za msingi zinazosaidia
mwajiri kumsimamisha mfanyakazi au mfanyakazi kuacha kazi ni sheria ya
ajira na mahusiano kazini.
"Waajiri wafuate utaratibu endapo
wanataka kuahirisha kazi kwa mwajiriwa au kumsimamisha ili kuepusha
migogoro inayoweza kujitokeza," amesema Kibona.
"Wafanyakazi
wengi wanaachishwa bila kufuata utaratibu na imesababisha kuwa na kesi
nyingi mahakamani hivyo, ni lazima kufuata utaratibu wa kumwachisha
mfanyakazi anapokuwa kazini kupata haki zake na kupunguza kuongezeka
kwa kesi hizo," amesisitiza Kibona.
Windi Clement ambaye ni
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi SS Tanzania Limited amesema mafunzo hayo
yatamsaidia kuboresha mahusiano mema kwa wafanyakazi na waajiri na
kutetea wafanyakazi kuhakikisha wanapata haki zao.
Amesema
viwanda vingi vinachangamoto ya mikataba kwani asilimia kubwa hutoa
mikataba ya mwaka mmoja hivyo, haiwapi nguvu wafanyakazi kuweza
kupambana kufanya kazi za uzalishaji.
Pia amesema uwepo wa
kampuni tanzu ndani ya kampuni moja husababisha kukosekana kwa
uwakilishi wa vyama vya wafanyakazi na hivyo, kusababisha wafanyakazi
wengine kunyanyasika.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Ilala, Vicky Kibona,akizungumza na waandishi wa habari namna mafunzo kwa wafanyakazi kutambua haki zao za ajira kazini yatakavyokuwa na manufaa kwao.Baadhi ya wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali binafsi na zile za umma wa wakiwa katika mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo kutambua haki zao leo jijini Dar es Salaam.
Bundi Clement, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi kiwanda cha Pepsi nchini, akizungumza baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ya siku moja kwa wafanyakazi wa a sekta binafsi na Umma ya kuwajengea uwezo kutambua haki zao za yaliyotolewa na WLAC leo Februari 12, 2021 jijini dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment