Mshindi wa Shindano la Vipaji Benki ya CRDB atinga Tamasha la Sauti za Busara - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 12, 2021

Mshindi wa Shindano la Vipaji Benki ya CRDB atinga Tamasha la Sauti za Busara

 

Richard Nchimbi maarufu kama Mucho flows (katikati mwenye miwani) ambaye aliibuka mshindi katika shindano la vipaji lililoendeshwa na Benki ya CRDB kupitia mitandao ya kijamii ametinga Zanzibar kujumiaka na maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi wanaoshuhudia tamasha la Sauti za Busara lililoanza rasmi leo tarehe 12 hadi 13 Februari, 2020.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mucho ameishukuru Benki ya CRDB kwa fursa hiyo ambayo ameipata ambayo imesaidia kumtambulisha yeye binafsi na kipaji alichonacho. Mucho anasema shindano lililoandaliwa linaonyesha ni jinsi gani benki hiyo imedhamiria kuwawezesha vijana kupitia kuendeleza vipaji vyao.".... kipaji ni ajira na sasa hivi kuna mwamko mkubwa wa vijana kutumia vipaji vyao kujiendeleza kimaisha, niipongeze Benki ya CRDB kwa kuliona hili," anasisitiza Mucho.

Mbali na kuhudhuria tamasha la Sauti za Busara, Mucho pia amepata kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Zanzibar ikiwamo mji mkongwe, msitu wa jozani na kisiwa cha changuu.
"Nimefurahi kupata fursa pia ya kutembelea vivutio vya utalii.. hii imenifanya kuijua zaidi nchi yangu na kunifanya kuwa mzalendo zaidi," anaongezea Mucho.

Akimtambulisha mshindi huyo kwa Waandishi wa habari, Meneja wa Benki ya Tawi la Benki ya CRDB, Mbwana Ahmed amesema benki hiyo imeendelea kujikita katika kuendeleza vipaji vya vijana kama njia ya kuwawezesha vijana kukua kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.

"Kama mnavyojua Benki yetu ni moja ya wadhamini wa tamasha la Sauti za Busara, hili ni tamasha la kuonyesha vipaji, hivyo basi tukaona tutumie fursa hii kuonyesha vipaji vya vijana wetu na kuwafungulia njia," alisema Mbwana.
Mbwana anasema Benki ya CRDB imeitumia fursa hiyo pia kutangaza utalii wa ndani kama sehemu ya mkakati wake katika kuisaidia Serikali kuhamasisha utalii wa ndani. “..mbali na Mucho pia tuna washindi wengine watatu kutoka matawi yetu katika mikoa Manyara, Shinyanga na Arusha ambao wamejishindia kutokana na idadi ya miamala ya TemboCradVisa,” alisema Mbwana.

Benki ya CRDB inatumia tamasha hilo la Sauti za Busara pia kutoa elimu juu ya matumizi ya mifumo ya kidijatali ya huduma za kibenki ikiwamo SimBanking, Internet banking, SimAccount, TemboCardVisa na CRDB Wakala ambapo wateja wamekuwa wakipata zawadi na punguzo katika manunuzi yao.

 "... tulianza na kuhamasisha wateja kwa kulipia tiketi zao kupitia njia hizi za kidijitali na sasa tunawaambia waendelee kufanya malipo popote pale kupitia njia hizi," anaongezea Mbwana huku akisisitiza kuwa matumizi ya mifumo ya kidijitali yanasaidia wateja kupata huduma kwa haraka, urahisi na kwa gharama nafuu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad