Ecobank yatoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa wa Kansa - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 5, 2021

Ecobank yatoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa wa Kansa


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ecobank Tanzania, Charles Asiedu(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu namna Benki hiyo ilivyoshiriki kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa Kansa wakati wa maadhimisho ya kansa Duniani yanayofanyika kila tarehe 04 mwezi Februari kila mwaka. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu akitoa ufafanuzi baadhi ya mambo yanayohusu benki hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari waliofika makao makuu ya Benki hiyo iliyopo Kinondoni jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ecobank Tanzania, Charles Asiedu.
 

 ECOBANK Tanzania kwa kushirikiana na taasisi na asasi za kiraia ikiwemo Kampuni ya Chief Promotions wameungana katika kutoa elimu ya uelewa kwa Serikali na Umma wa watanzania pamoja na kutoa misaada ya vifaa vya shule,Vipima Joto, Maziwa ya Unga,Sabuni, Pampasi, Dawa za meno, miswaki  pamoja na Mafuta ya Kupaka kwa Watoto wenye matatizo ya Kansa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Kansa duniani Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ecobank Tanzania, Charles Asiedu ameeleza kuwa saratani hukatiza maisha ya maelfu ya watanzania kila mwaka na benki hiyo imeendelea kutoa elimu ya uelewa kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza kupitia kampeni yao ya miaka mitatu ambayo kwa kiasi kikubwa wametoa elimu ya Afya na kubadili mitindo ya maisha.

"Kupitia kampeni yetu ya Kupambana na magonjwa yasiyoambukiza Ecobank tumekuwa tukihimiza kuzingatia chakula bora, kufanya mazoezi, kutovuta sigara na  kupunguza unywaji wa pombe." alisema Asiedu .
 
Amesema kuwa katika maadhimisho ya uelewa katika siku ya saratani duniani Ecobank itafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa msaada wa watoto waliothirika na saratani katika hospitali ya taifa Mhimbili pamoja na kutoa jumbe mbalimbali za uelewa wa kansa kupitia Televisheni, Redio na mitandao ya kijamii ili kujenga uelewa zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko katika Benki hiyo, Furaha Samalu amesema wataendelea kutoa elimu juu ya ugonjwa huo, kuelimisha Jamii na kuhimiza Jamii kula Milo ya Kiafya ili kujikinga na maambukizi ya Kansa.

“Sisi tunafahamu Ugonjwa wa Kansa ni zaidi ya Ukimwi, Malaria na hata COVID-19, hivyo sisi tunawapenda Watanzania wote na watu wote duniani wachukue tahadhari kujinga na Kansa”, amesema Samalu.

Tafiti zinaonesha kuwa watu milioni kumi hufariki kwa tatizo la saratani kote ulimwenguni huku ikielezwa kuwa vifo hivyo ni zaidi ya vile vinavyosababishwa na UKIMWI na Malaria, na inakadiliwa kuwa hadi kufikia 2030 vifo vitikanavyo na saratani vitafikia milioni 13 kama hatua madhubuti hazitachukuliwa.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad