JOYCE KIRIA ASHIKILIWA NA POLISI DAR - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 5, 2021

JOYCE KIRIA ASHIKILIWA NA POLISI DAR

 
 

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wanamshikilia mwanaharakati Joyce Kiria kwa kosa la kuendesha mtandao wa Youtube bila kuwa na leseni.

Hatua hiyo ni muendelezo wa Mamlaka hiyo katika kudhibiti  Mawasiliano kwa watu wanaondesha maudhui kwa njia ya Mtandao, pamoja na  kutoa elimu kwa watu wanaoendesha maudhui mtandaoni kujisajili katika Mamlaka hiyo.

Mbali na Joyce Kiria TCRA kwa kushirikiana na polisi wamemkamata  mtu mmoja  kwa kuendesha Chaneli ya Youtube bila usajili.

 Joyce Kiria anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad