Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Mindi Kasiga (Kulia) akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez akiwa pamoja na Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara, kuhusiana na majukumu ya Bodi ya Utalii Tanzania na jinsi watakavyoweza kushirikiana katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kupitia michezo.
Katika picha ya pamoja wakati wa mazungumzo
……………………………………………………………….
Viongozi wa timu ya Mpira wa miguu ya Klabu ya Simba, leo tarehe 25/1/2021 wametembelea ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jijini Dar es Salaam kwa lengo kuangalia namna watakavyoweza kushirikiana na Bodi katika kutangaza utalii wa Tanzania kupitia Michezo. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa TTB.
No comments:
Post a Comment