Naibu
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini kutoka Tume ya Maendeleo ya
Ushirika,Charles Malunde akisistiza jambo wakati wa mkutano huo kulia ni
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Tanga, Jackline Senzighe
Naibu
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini kutoka Tume ya Maendeleo ya
Ushirika,Charles Malunde akisistiza jambo wakati wa mkutano huo kulia ni
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Tanga, Jackline Senzighe
Sehemu
ya wadau wakiwemo viongozi wa chama cha ushirika na ufugaji ambavyo
vimeunda chama kikuu cha ushirika wa maziwa Tanga wakimsikiliza kwa
umakini Naibu Mrajisi wa vyama ushirika kutoka Tume ya Maendeleo ya
Ushirika
Mmoja wa wanaushirika akiuliza swali katika mkutano huo
Naibu
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini kutoka Tume ya Maendeleo ya
Ushirika,Charles Malunde amewataka wafugaji kubadilikana watoke kwenye
ufugaji wa mazoezi badala yake wafuge kisasa ili waweze kupata manufaa
makubwa yanayotokana na eneo hilo.
Malunde aliyasema hayo mjini
Tanga wakati alipokutana na viongozi wa chama cha ushirika na ufugaji
ambavyo vimeunda chama kikuu cha ushirika wa maziwa Tanga wakati wa
ziara yake.
Alisema wafugaji hao wanapaswa kubadilika kutokana
na alichobaina kwenye ziara yake kuna wafugaji kwa ng’ombe wanapata lita
nne kwa sababu ya matunzo mabaya na yanapokuwa matunzo mazuri yule
ngombe anabadilika anatoka kwenye lita nne hadi ishirini.
Malunde
alisema kwa hiyo ukiangalia wakati fulani mfugaji anaangalia
anachokipata kutokana na kile alichowekeza lakini kumbe tatizo linakuwa
kutokana na matunzo mabaya ndio maana uzalishaji wa maziwa umekuwa
kidogo.
“Kuna mambo tumejadilia hapa ikiwemo suala la bei..bei
wakati wote imeonekana sio rafiki kwa mfugaji lakini ahadi ambayo
nimeitoa pamoja na hili ambalo linaweza kuangaliwa lakini wafugaji
wenyewe waone kuna haja ya kuangalia namna ya utunzaji bora kuwalisha
vizuri mifugo ili waweze kupata maziwa mengi”Alisema
Hata hivyo
alisema suala jingine namna ya kupata mitamba bora bila kuingia kwenye
mikopo huku akitolea mfano kwa wafugaji hao kwamba wakiwekeza kila siku
lita tano za maziwa wanazotoa baada ya mwaka mmoja zitakuwa
zimetosheleza kununua mtamba mmoja.
Aliongeza kwa hiyo kwa
sababu ya serikali na tume ya maendeleo ya Ushirika wamehamasisha
kuundwa sacoos mahali penye amcos hivyo ametoa wito waendelee
kuliangalia hilo kuna uwezekano mkubwa wa kupata mitamba kwa kudunduliza
kwao bila kuhitaji taratibu za kupata mikopo.
Alisema kutokana
na kwamba inachukua muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja mpaka miaka miwili
kama ni hivyo kupitia kwenye hizo taratibu zao kuna uwezekano
wakaanzisha huo utaratibu mitamba inaweza kupatikana ndani ya miezi sita
wakati atakapokuwa akiendelea kudunduliza maziwa yake huo ni mfano.
Katika
hatua nyengine aligusia suala la wafugaji ambao wanaondoka na kwenda
kuuzia sehemu nyengine ambapo alitoa onyo vyama vya ushirika kuacha
kufanya hivyo mara moja.
“Kuna chama cha ushirika ambacho
kimeonekana kukusanya maziwa ya mfugaji kwa bei fulani halafu kinakwenda
kuuza sehemu nyengine viongozi ambao wameonekana kufanya hivyo ameagiza
wale maafisa ushirika sehemu walipo wawachukulie hatua ikiwemo
kuwaondoa kwenye nafasi zao”Alisema
Alisema wachukua maamuzi
hayo ili kusudi ikawe fundisho kwa wenzao kwa sababu lengo lilikuwa
wakikisanya wanaunganisha nguvu ya pamoja lakini hao wanachukua maziwa
na kwenda kuuza maeneo mengine pembeni hiyo ni hujumu.
Malunde
alisema kwa namna hiyo na kwa kufanya hivyo wanausaliti ushirika
ulioundwa na wao kama wanausimamia wanawaona hawafai na kwa sababu kama
bado wapo viongozi ambao wanawasaidia hao ndio wanawahitaji warudi na
kubadilishwa viongozi wengine ambao wanaweza kuusimamia ushirika.
Awali
wakizungumza katika mkutano huo Mwanahawa Hiza kutoka Chama cha
Ushirika cha Uviwaki Pingoni Jijini Tanga alisema kwamba wao changamoto
yao ni kipindi cha ukame maziwa yanakuwa madogo na hayapatikani.
Alisema
lakini kipindi cha mvua wakati wa kuchukua maziwa kuyapeleka mjini kuna
maeneo mengine korofi na hivyo kuwa na changamoto.
Aidha
alisema pia bei ya maziwa sio nzuri maziwa wanauza lita sh.820
wakiwaambia waongeze bei wanasema bei ni hiyo hiyo huku malisho ya
ngombe yakiendelea kuwa ghali.
“Kipindi cha mvua kutoa Maziwa
eneo la Pingoni Kata ya Pongwe hadi mjini Tanga kuna maeneo magari
yanakwamba na hivyo kufanya ucheleweshwaji wa fedha”Alisema
Aliomba
serikali iangalie suala la bei kutokana na kwamba wafugaji wanateseka
waweze bei ya uwiano kwa pamoja na haiwezi kukaa hivyo hivyo miaka yote.
Monday, December 14, 2020
Home
HABARI
NAIBU MRAJISI WA VYAMA VYA USHIRIKA MALUNDE AWATAKA WAFUGAJI KUBADILIKA NA KUACHA UFUGAJI WA MAZOEA
NAIBU MRAJISI WA VYAMA VYA USHIRIKA MALUNDE AWATAKA WAFUGAJI KUBADILIKA NA KUACHA UFUGAJI WA MAZOEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment