HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 2, 2020

MAONESHO YA TANO YA BIDHAA ZA VIWANDA VYA TANZANIA KUFANYIKA BILA VIINGILIO

 

Naibu Mkurugenzi mkuu wa Mmlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania (Tan Trade,) Latifa Khamis akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maonesho ya tano ya bidhaa za viwanda vya Tanzania na kusema kuwa Tanzania ina bidhaa zenye viwango bora na zinaweza kushindana kimataifa. Leo jijini Dar es Salaam.


Maandalizi ya maonesho ya Tano ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yakiendelea.
 
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

WIZARA ya Viwanda na Biashara kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade,) imeandaa maonesho ya tano ya bidhaa za Tanzania yatakayofanyika kuanzia Desemba 3 hadi 9 ikiwa ni katika kuhakikisha ujenzi wa uchumi wa viwanda unakuwa na matokeo chanya katika uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade  Latifa Khamis amesema kuwa maonesho hayo yanayokwenda na kauli mbiu ya "Tumia Bidhaa za Tanzania, Jenga Tanzania." Imelenga kuhamasisha watanzania kuwa wazalendo pamoja na kupenda na kununua bidhaa za nyumbani.

Amesema katika maonesho hayo ambayo hayana viingilio, Desemba 5 Tan Trade na taasisi nyingine dhibiti zitakutana na wadau wakiwemo wamiliki wa viwanda na kujadiliana masuala mbalimbali ya kuboresha na kutatua changamoto zinazowakabili.

Amesema, maonesho hayo yataambatana na matembezi ya Afya, mashindano mbalimbali na uhamasishaji wa bidhaa za maziwa ambapo watembeleaji watapata fursa ya kuonja maziwa katika viwanda vyote vya maziwa nchini.

Aidha, amesema maonesho hayo yatakwenda sambamba na mikutano na balozi mbalimbali za nje ya nchi  itakayolenga kutafuta fursa.

Pia amewataka watanzania kushiriki maonesho hayo na kuona bidhaa ambazo zina viwango vya kimataifa na zinaweza kushindana kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad