MSAJILI WA MAHAKAMA YA KIMBARI AAHIDI USHIRIKIANO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 2, 2020

MSAJILI WA MAHAKAMA YA KIMBARI AAHIDI USHIRIKIANO

 

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kulia) akimsikiliza Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari ‘IRMCT’, Bw. Abubacarr Tambadou. Bw. Tambadou ambaye alichaguliwa rasmi Julai mosi, 2020 amemtembelea Mhe. Jaji Mkuu kwa lengo la kujitambulisha na kuimarisha uhusiano.
Mazungumzo yakiendelea, kushoto ni Bi. Tully Mwaipopo, Mwanasheria kutoka Mahakama hiyo.
Picha ya pamoja.

Na Mary Gwera, Mahakama

MSAJILI wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari ‘IRMCT’, Bw. Abubacarr Tambadou ameahidi kuendeleza ushirikiano wa utendaji kazi baina ya Mahakama hiyo na Mahakama ya Tanzania.

Akizungumza wakati alimpotembelea Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ofisini kwake leo Desemba 02, 2020, Msajili huyo alisema kuwa yupo tayari kuendeleza kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na ‘IRMCT’ kwa maslahi ya Taifa.

 “Nina furaha kukubali ombi langu la kuonana na wewe licha ya kuwa na majukumu mengi ya kazi, lengo la mimi kuja kukutembelea ni kujitambulisha rasmi na kuomba kuendeleza ushirikiano wa kikazi baina yetu,” alieleza Bw. Tambadou.

Vilevile, Bw. Tambadou alieleza kuwa Mahakama ya Tanzania itumie vyema uwepo wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari ‘IRMCT’ kama tija ya kujua zaidi sheria za kimataifa.

Naye, Mhe. Jaji Mkuu alimuahidi Msajili huyo kutoa ushirikiano zaidi na kuahidi kumtembelea pindi atakapokuwa Arusha.

Aidha; Mhe. Jaji Mkuu alipataa wasaa wa kumueleza Msajili huyo kuwa Mahakama ipo katika maboresho mbalimbali yanayolenga kurahisisha na kusogeza huduma za haki karibu zaidi na wananchi.

Hali kadhalika Mhe. Jaji Prof. Juma alimueleza Bw. Tambadou kuwa Mahakama ya Tanzania kwa sasa ipo katika maandalizi ya kuadhimisha miaka 100 ya kuanzishwa kwa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Bw. Abubacarr Tambadou alichaguliwa kuwa Msajili wa Mahakama hiyo Julai mosi mwaka huu.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad