CSI WAENDELEA KUTOA ELIMU KUHUSU AFYA YA MAMA NA MTOTO ILI KUPUNGUZA VIFO VINAVYOTOKEA WAKATI WA KUJIFUNGUA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 6, 2020

CSI WAENDELEA KUTOA ELIMU KUHUSU AFYA YA MAMA NA MTOTO ILI KUPUNGUZA VIFO VINAVYOTOKEA WAKATI WA KUJIFUNGUA


 Na Said Mwishehe

SHIRIKA la Childbirth Survival International(CSI) ambalo linajihusisha na afya ya Mama na Mtoto hasa katika kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi kwa mama na mtoto wakati wa kujifungua na vifo cha watoto wenye umri chini ya miaka mitano limesema litaendelea kuzungumzia umuhimu wa jamii kushiriki kikamilifu kupunguza vifo vinavyotokea wakati wa kujifunga.

CSI limesema hayo leo Desemba 6, 2020 jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kukabidhiwa fedha kwa Shule ya Msingi Sinza Maalum ambazo zitakwenda kufanikisha ujenzi wa vyoo na bafu kwenye shule hiyo ambayo kuna wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Hivyo pamoja na wadau wengine wa maendeleo kushiriki katika tukio hilo CSI kutokana na umuhimu wao kwenye jamii nayo ilipewa nafasi ya kushiriki na kutoa elimu ya afya ya uzazi ambayo itasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Uchangishaji wa fedha hizo kiasi cha Sh.milioni 11 umefanywa na Amka Twende Golden Women ambayo ipo chini ya Kampuni ya Open_Kitchen ambayo imejikita kuwawezesha na kuwasaidia wanawake wajasiriamali chini ya Mkurugenzi wake Upendo Mwalongo kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo.

Akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo maofisa kutoka serikalini, wadau wa maendeleo , wanawake wajasiriamali , Mwakilishi kutoka CSI ambaye ni Meneja wa Programu za Vijana katika shirika hilo Ester Mpanda amefafanua wanajihusisha na afya ya mama na mtoto na lengo ni kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifunga na wale wenye umri chini ya miaka mitano.

Amesema CSI makao makuu yake yapo nchini Marekani lakini wanayo ofisi yao nchini Tanzania pamoja na matawi mengine kaika nchi za Rwanda na Kenya na lengo kuu ni kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinapungua au kwisha kabisa.

"CSI mbali ya kuwa Marekani iko pia Tanzania, ni shirika la kimataifa ambalo limeanzishwa na wamama wawili ambao ni Tausi Swed Kagasheki ambaye anaishi Marekani na mama Stella Mpanda ambaye yuko nchini Tanzania.

"Tuko hapa kwenye Amka Twende kwasababu tunaona ni nafasi kwetu sisi kuzungumzia masuala yanayohusu afya ya mama na mtoto ambayo tunaamini inawahusu na akina , suala la afya ya mama na mtoto sio la mama peke yake bali na baba naye anahusika maana sote tunahusika katika kuhakikisha maisha ya mama na mtoto yanakuwa salama,"amesema Ester Mpanda.

Ameongeza hivyo wanamshukuru Upendo Mwalongo kwa kuwapa nafasi hiyo ya kuungana na Kampuni ya Open_ Kitchen inayosimamia mradi wa Amka Twende na timu yake ili kuzungumzia kwa kina kuhusu shirika hilo na majukumu yake.Pia amesema CSI inapongeza na kuishukuru Serikali kwa jitihada zake za kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo shirika hilo la kimataifa.

Ester Mpanda kupitia meza yao ya kutoa elimu iliyokuwepo kwenye eneo hilo, ilikuwa na jukumu la kuhakikisha elimu kuhusu usalama wa afya ya mama na mtoto inawafikia wageni waliokuwa wamehudhuria na miongoni mwa waliopata nafasi ya kufika kwenye meza ya CSI ni mgeni rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kijitonyama Dama Lusangija.

Kwa upande wake Upendo Mwalongo alipata nafasi ya kumtambulisha Ester Mpanda kwa wadau mbalimbali wa maendeleo waliohudhuria tukio hilo la ukabidhiwaji fedha huku akionesha kufurahishwa na kile ambacho CSI wanafanya katika jamii kuhakiksha vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua na vile vya watoto chini ya miaka mitano vinakwisha.

Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Kijitonyama Dama Lusangija(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Programu za Vijana katika shirika la Childbirth Survival International(CSI) Ester Mpanda kuhusu kazi zinazofanywa na Shirika hilo hasa hasa katika kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi kwa mama na mtoto wakati wa kujifungua na vifo cha watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa tukio la kukabidhiwa fedha kwa Shule ya Msingi Sinza Maalum ambazo zinakwenda kufanikisha ujenzi wa vyoo na bafu kwenye shule hiyo ambayo kuna wanafunzi wenye mahitaji maalum ziilizochangishwa na Kampuni ya Open_ Kitchen.Meneja wa Programu za Vijana katika shirika la Childbirth Survival International(CSI) Ester Mpanda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyohamasika kudhamini  pamoja na kutoa elimu kuhusu makuzi ya mtoto hasa katika kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi kwa mama na mtoto wakati wa kujifungua na vifo wakati wa tukio la kukabidhiwa fedha kwa Shule ya Msingi Sinza Maalum ambazo zinakwenda kufanikisha ujenzi wa vyoo na bafu kwenye shule hiyo ambayo kuna wanafunzi wenye mahitaji maalum ziilizochangishwa na Kampuni ya Open_ Kitchen .Meneja wa Programu za Vijana katika shirika la Childbirth Survival International(CSI) Ester Mpanda akitoa elimu kwa baadhi ya wanawake waliofika kwenye hafla ya kukabidhiwa fedha kwa Shule ya Msingi Sinza Maalum ambazo zinakwenda kufanikisha ujenzi wa vyoo na bafu kwenye shule  hiyo ambayo kuna wanafunzi wenye mahitaji maalum ziilizochangishwa na Kampuni ya Open_ Kitchen.Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Kijitonyama Dama Lusangija akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya kijamii mara baada ya kukabidhi fedha kwa Shule ya Msingi Sinza Maalum.Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Kijitonyama Dama Lusangija  akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa shirika la Childbirth Survival International(CSI)  pamoja na uongozi wa Kampuni ya Open_ Kitchen.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad